Biden ateta na washauri wa usalama Marekani

Rais mteule wa Marekani, Joe Biden amekutana na washauri wake wa usalama wa taifa katika mkutano ambao haukuhudhuriwa na wataalam wa upelelezi wa serikali, wakati Rais Donald Trump anaendelea kuzuia mchakato wa kipindi cha mpito.
Biden na Makamu wake Kamala Harris wamejadili kuhusu masuala mbalimbali ulimwenguni katika mkutano huo na maafisa wa ujasusi na wataalam wa ulinzi.

Kati ya waliohudhuria mkutano huo ni aliyekuwa Naibu wa Waziri wa Mambo ya Nje, Tony Blinken, waliokuwa mabalozi wa Marekani Nicholas Burns na Samantha Power, jenerali mstaafu Stanley McChrystal na wengine wengi.

Siku za karibuni,wabunge kadhaa wa chama cha Republican wamesema kwamba maafisa ujasusi wa serikali, wanastahili kutoa taarifa hizo kwa Biden, kuelekea Januari 20,2021 siku ambayo anatarajiwa kuapishwa kuwa Rais wa 46 wa Marekani.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news