FIFA yamfungia miaka mitano Rais wa Shirikisho la Soka Afrika

Bodi ya Uendeshaji Michezo ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) imemfungia miaka mitano Rais wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Ahmad Ahmad kutojihusisha na mchezo wa soka na shughuli zote zonazohusiana na mchezo huo.
Kamati ya Nidhamu ya FIFA imesema Ahmad alikuwa na matumizi mabaya na ufujaji wa fedha za CAF akiwa madarakani. Rais huyo mwenye miaka 60 taarifa zinaeleza kuwa amekuwa kwenye uvunjifu wa taratibu zilizowekwa na kwenye masuala ya matumizi ya fedha kwa muda mrefu kwenye masuala ya fedha.

"Uchunguzi juu yake umefanywa kwa muda mrefu na ulianza baada ya kuingia madarakani mwaka 2017-2019, kuna mambo yalikuwa hayapo sawa kwenye masuala ya mipango na matumizi,"ilieleza taarifa ya Kamati hiyo.

Post a Comment

0 Comments