Health Summit kufanyika jijini Dodoma Novemba 25 hadi 26

Jumla ya wadau 354 katika sekta ya Afya nchini wanatarajia kushiriki Kongamano la Afya la Tanzania Health Summit linalotarajia kufanyika jijini Dodoma Novemba 25 hadi 26, mwaka huu,anaripoti Doreen Aloyce (Diramakini) Dodoma.

Daktari Omary Chillo akielezea maandalizi ya kongamano la afya litakaloambatana na maonyesho jijini Dodoma. (Diramakini).

Rais wa Kongamano la Afya la Tanzania Health Summit, Dkt. Omary Chillo amesema hayo leo Novemba 23, 2020 wakati akizungumza na waandishi wa habari huku akisema kongamano hilo ni la saba kufanyika na lengo ni kujadili uchumi wa kati unavyoendana na sekta ya afya.

Dkt.Chillo amesema, katika kongamano hilo taasisi zisizo za kiserikali zitatoa mada na kujadili ni jinsi gani hasa wataweza kuboresha afya ya jamii kwa wananchi wote nchini Tanzania.

Pia ameongeza kuwa, katika mkutano huo watatoa mrejesho wa mikutano mingine iliyowahi kufanyika na kutoa mapendekezo ya nini hasa kifanyike katika kuboresha sekta ya afya kipindi hiki cha uchumi wa kati.

Amesema, malengo makuu ya kongamano hilo ni kubadilisha uzoefu na kuona wanafanyaje kazi hasa kipindi hiki tulichoingia uchumi wa kati katika la Tanzania.

"Kutakuwepo na maonyesho mbalimbali ya masuala ya afya na wabunifu watakoshiriki katika kongamano hilo watapatiwa zawadi,"amesema Dkt. Chillo.

Ametoa wito kwa watu ambao bado hawajajiandikisha kujiandikisha ili washiriki pamoja katika kongamano hilo ili kuleta chachu katika sekta ya afya na kuboresha mifumo ya afya nchini.

Katika kongamano hilo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Prof.Magula Mchembe na atakayefunga anatarajiwa kuwa Katibu Mkuu Mhandisi Joseph Nyamhanga kutoka Ofsi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news