Goli la Yanga SC lamng'oa kocha Azam FC

Baada ya ushindi wa Novemba 25, 2020 ambao Yanga SC iliuchukua nyumbani kwa Azam FC katika uwanja wao wa Azam Complex uliopo nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam, wachambuzi wa soka wameidokeza Diramakini kuwa, ndiyo chanzo cha kung'olewa kocha wa Azam FC, Aristica Cioaba katika msimu wa 2020/2021, anaripoti Mwandishi Diramakini.

Aidha, uongozi wa Azam FC kupitia kwa Ofisa Habari, Zakaria Thabit umesema kuwa mchakato umefanyika kuanzia timu ilipopoteza mchezo wa kwanza dhidi ya Mtibwa Sugar na mechi zilizofuata timu ilicheza chini ya kiwango.


"Timu imekuwa ikicheza chini ya kiwango baada ya kupoteza mbele ya Mtibwa Sugar, hata tuliposhinda mbele ya Dodoma Jiji bado hakukuwa na kiwango bora. Kwenye mchezo wetu wa jana dhidi ya Yanga hali ilikuwa hivyo na tumepoteza hivyo makubaliano ya pande zote mbili tumefika makubaliano na kwa sasa Vivier Bahati atakuwa Kaimu Kocha Mkuu," amesema.

Katika mchezo huo wa Ligi Kuu Tanzania Bara (VPL) uliochezwa kwenya uwanja huo goli pekee la Yanga SC lilifungwa na Deus Kaseke dakika ya 48 akimalizia pasi ya mshambuliaji, Yacouba Sogne.

Ushindi huo uliwaweka Yanga kileleni mwa Msimamo wa Ligi baada ya kufikisha alama 28 na kuwashusha Azam FC kwenye nafasi ya pili wakiwaa na na alama zao 25.

Aidha, mbali na kukaa kwenye kilele cha msimamo wa Ligi Kuu, lakini pia ushindi huo uewafanya Yanga SC kuwa wababe wa Azam kwani katika mechi 25 walizokutana wameshindanda mechi tisa dhidi ya nane za Azam FC huku wakitoka sare kwenye mechi nane.

Yanga pia wameendelea kuweka rekodi bora msimu huu kwani hadi sasa zikiwa zimeshachezwa mechi 12, ni timu pekee ambayo haijapoteza mchezo wowote wakipata sare jatika mechi nne na kushinda mechi nane.

Kocha Mkuu wa Yanga, Cedric Kaze amesema kuwa walistahili kushinda mchezo kwani kikosi chake kilicheza vizuri kunzia kwenye kuzuia na eneo la kati ingawa bado kuna shida kwa washambuliaji kwani walikuwa na uwezo wa kupata goli zaidi ya moja.

Kaze amesema, bado inamuumiza kichwa kuona wanendelea kupata ushindi mwembamba wa goli moja hivyo anapaswa zaidi kulifanyia kazi jambo hilo kwa kuwafanya wachezaji kujiamini ili kutumia ipasavyo nafasi za magoli wanazotengeneza.
Pia kocha huyo amesema kuwa, kinachompa matumaini kwa sasa ni wachezaji wake kucheza kwa muunganiko zaidi tofauti na ilivyokuwa awali na jambo hilo linaonesha wazi kuwa wameanza kurejesha kujiamini hata kwenye eneo la hatari.

Hata hivyo, kocha wa Azam FC ambaye ameng'olewa, ndugu Cioaba amesimamia kwenye mechi 12 ambapo amepata ushindi mechi nane, sare moja na kupoteza tatu.

Post a Comment

0 Comments