Mashindano ya wazi ya TPC Golf yatimua vumbi

Wachezaji wa ridhaa wa mchezo wa gofu zaidi ya 70 wamesheriki mashindano ya wazi ya TPC yanayoendelea katika viwanja vya Kiwanda cha Sukari cha TPC kilichopo Moshi mkoani kilimanjaro, anaripoti Mwandishi Diramakini.

Akizungumza wakati wa kuanza kwa mashindano hayo, Nahodha wa Klabu ya Golf ya TPC, Jaffary Iddi amesema kuwa, malengo ya mashindano hayo ni kukuza mchezo huo huku idadi ya wachezaji ikiwa ni faraja kubwa kwao.

"Tunaendelea kukuza mchezo, hatua si mbaya tuna vijana wengi sasa wanacheza, tunaamini baada ya muda mfupi tutakuwa na wachezaji wengi wazuri kwa maslahi ya Taifa letu,"amesema.

Nahodha huyo amesema kuwa, pia programu ya watoto imekuwa na tija na imekuwa kipaumbele, hivyo wanatarajia kuendesha mashindano makubwa ili kuendelea kutoa hamasa.

"Unajua kufanyika kwa mashindano haya kwa wingi, kwana hutoa hamasa kwa wenyeji kujiandaa na wengine wanaozunguka kuhamasika na mchezo,"ameongeza Jaffary.

Naye mchezaji namba moja wa klabu hiyo, Ally Mcharo amesema kuwa, matumaini yake ni makubwa kwani kiwanja anakijua viruzi.

Mcharo ambaye kiwango chake cha uchezaji ni zaidi ya fimbo tano amesema, baada ya mafanikio ya mashindano ya ndani anatarajia klabu itampa fursa zaidi Kimataifa.

Kwa upande wa wanawake, mchezaji Hadija Selemani wa Lugalo amesema kuwa, mchezo ni mgumu, lakini kwa kuwa ni mchezo wa siku mbili anaamini atafanya vizuri.

Bi.Hadija ni miongoni mwa wachezaji 10 wa Lugalo wanaoshiriki mashindano hayo wakiwemo wachezaji wengine kutoka Arusha Gymkhana, Moshi na Kili Golf.

Mashindano haya ya wazi ni ya TPC ni ya siku mbili kwa wachezaji wa ridhaa na wa kulipwa yanatarajiwa kuhitimishwa leo wakati kwa wachezaji wa kulipwa yalihitimishwa jana baada ya kuanza Ijumaa.

Post a Comment

0 Comments