Mo Dewji:Mukoko Tonombe si kipaumbele chetu kwa sasa

Mohamed Dewji (Mo Dewji) ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Klabu ya Simba amesema suala la Simba kuwa inamuwania kiungo nyota wa Yanga, Mukoko Tonombe ni propaganda zilizotengenezwa, anaripoti Mwandishi Diramakini.
Dewji ameyasema hayo leo Novemba 15, 2020 wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Saalam huku akisisitiza kuwa, Simba haijawahi kumjadili Mukoko na wala haina habari naye kama inavyoelezwa mitandaoni.

Amesema, kocha ndiye anependekeza mchezaji gani anatakiwa, "huyo mchezaji (Mukoko) hatujawahi kumjadili,"amesema Dewji.

Pia Dewji amekiri kuwa, Kocha Sven van der Broeek amependekeza kusajiliwa kwa kiungo mkabaji kutokana na Gerson Fraga kuwa majeruhi kwa muda mrefu sasa.

Dewji ameendelea kusisitiza kwamba suala lao la kumsajili kiungo mkabaji litakuwa ni siri."Hiyo ni siri, si kwamba tunazihofia timu za hapa ndani. Lakini tunahofia pia hata zile za nje ya Tanzania kwa kuwa kutokana na mwendo mzuri wa Simba, kumekuwa na ushindani mkubwa sana,"amesema.

Post a Comment

0 Comments