Mo Dewji ahitimisha mjadala wa Chama kuhamia Yanga SC

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Simba, Mohamed Dewji amesema klabu hiyo ilishaingia mkataba mpya na kiungo Cleotus Chama na unaisha mwaka 2022, hivyo taarifa za kuwa anakwenda Yanga SC zimekuwa zikiwashangaza, anaripoti Mwandishi Diramakini.
  
Dewji ameyasema hayo leo Novemba 15, 2020 wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam. Bilionea huyo kijana amesema kuwa,mchezaji huyo ni mali ya Simba SC na hakuna sababu ya kuwa na hofu kumuhusu yeye.
“Taarifa sijui anakwenda Yanga ni mambo ambayo si sahihi, hakuna sababu ya kuwa na hofu na ninawatoa hofu mashabiki wa Simba kuwa tuko makini sana. Sehemu mbalimbali zimekuwa nikikutana na mashabiki wa Simba ambao wananiambia Mo fanya Chama asiondoke Simba. Chama ni mchezaji wa Simba.

“Suala kwamba anakwenda Yanga sijui linatoka wapi, lakini haina shida, sasa nimewaambia na ninafikiri leo tunafunga mjadala,”amesema Mwenyekiti huyo.

Post a Comment

0 Comments