Simba SC haiwezi kumuachia Luis Miquissone asema Dewji

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Simba, Mohamed Dewji amesema kiungo nyota wa Simba SC, Luis Miquissone ana kandarasi ya miaka mitatu na nusu na klabu hiyo, anaripoti Mwandishi Diramakini.
Amewataka wana Msimbazi kutokuwa na hofu yoyote kuhusu nyota huyo kwa kuwa, wapo makini na nyota huyo.

Bilionea Dewji ameyasema hayo leo Novemba 15, 2020 mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

"Kama watahamia kwa Luis, sisi tuko makini sana na tunajua nini tunafanya. Mkataba wake ni miaka mitatu na nusu na hii tunaangalia kwa wachezaji vijana wenye future. Sioni kama kuna sababu ya kuwa na hofu, huyu ni mchezaji wetu na vizuri tuendelee na mambo mengine,"amesema Dewji.

Post a Comment

0 Comments