Mwalimu mbaroni kwa tuhuma za kubaka, kumlawiti mwanafunzi

Mwalimu wa Shule ya Msingi Montforty iliyopo Kola B, Manispaa ya Morogoro mkoani hapa anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kumbaka mwanafunzi wake wa darasa la tano, anaripori Victoria Kazinja (Diramakini) Morogoro.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Wilbroad Mutafungwa amesema, mwalimu huyo Eneza Anderson (27) mkazi Kihonda Viwandani anashikiliwa kwa kumbaka na kumlawiti mwanafunzi huyo mwenye umri wa miaka 10 mara kadhaa katika eneo la shule hiyo.

Kamanda Mutafungwa amesema, walipokea taarifa ya tukio hilo Novemba 5, mwaka huu majira ya saa sita mchana kutoka katika Ofisi za Dawati la Jinsia na Watoto Mkoa wa Morogoro.

Amesema, mwanafunzi huyo alipohojiwa alidai kuingiliwa kimwili na mwalimu wake huyo mara kadhaa maeneo ya ofisini na chooni wakati wanafunzi wenzake wanapokuwa darasani wakiendelea na masomo.

"Mtuhumiwa ni mwalimu wa taaluma katika shule hiyo na amekiri kumbaka na kumlawiti mara tano mwanafunzi wake," amesema Kamanda Mutafungwa.

Hata hivyo ,Mutafungwa amesema hatua za kumfikisha mahakamani mtuhumiwa huyo kwa kushirikiana na maafisa Ustawi wa Jamii zitafuata baada ya upelelezi kukamilika, na kutoa wito kwa wananchi kuacha vitendo vya ukatili kwa watoto, kwani vinavunja utu na kukatiza ndoto zao.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news