WACHEZAJI WA TIMU YA KMC FC WAWASILI KAMBINI

Wachezaji wa Timu ya Manispaa ya Kinondoni, KMC FC wamerejea kambini kwa ajili ya kuendelea kufanya maandilizi ya Ligi Kuu Soka Tanzania Bara 2020/2021 ikiwa ni baada ya kupewa mapumziko ya siku nne mara baada ya kurejea kutoka jijini Mwanza Novemba 5, mwaka huu, anaripoti Christina Mwagala (KMC FC).
Aidha, wachezaji ambao hawajarejea kikosini hadi sasa kwa sababu mbalimbali ni pamoja na Juma Kaseja, David Brayson ambao waliitwa katika timu ya Taifa ,Taifa Stars ,Hassan Kapalata, Rahim Sheih, Israel Mwenda ambao waliitwa katika kikosi cha Timu ya Taifa chini ya umri wa miaka 20 (Ngorongoro Heroes), pamoja na Keny Ally ambaye alifiwa na Baba yake mzazi.

Aidha, wachezaji hao wamerejea wakiwa katika hali nzuri na utaratibu wa kuanza kufanya mazoezi unafanyika na hivyo wakati wowote kuanzia sasa wataanza kufanya mazoezi kwa ajili ya kujiandaa na mchezo dhidi ya Namungo utakaochezwa mara baada ya kumalizika kwa michuano ya kimataifa.

“ Tumejipanga katika kipindi hiki ambacho ligi imesimama kwa muda ,tunawaandaa wachezaji wetu pindi tutakaporejea, tutahakikisha kuwa tunafanya vizuri katika michezo iliyopo mbele yetu tukianza na Namungo,"

Post a Comment

0 Comments