Rais Magufuli awateua Dkt.Shein,Mwakyembe, Kabaka

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amefanya uteuzi wa viongozi 3 kama ifuatavyo;

Kwanza, Mhe. Rais Magufuli amemteua Rais Mstaafu wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe.

Dkt. Shein anachukua nafasi ya Jaji Mstaafu Barnabas A. Samatta ambaye anamaliza muda wake.

Pili, Mhe. Rais Magufuli amemteua Dkt. Harrison Mwakyembe kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS).

Dkt. Mwakyembe anachukua nafasi ya Bi. Mariam Joy Mwaffisi ambaye amemaliza muda wake.

Tatu, Mhe. Rais Magufuli amemteua Bi. Gaudentia Mugosi Kabaka kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM)

Bi. Gaudensia Mugosi Kabaka anashika wadhifa huo kwa kipindi cha pili baada ya kipindi cha kwanza kumalizika.

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Mhe. Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi wa viongozi hao umeanza leo tarehe 24 Novemba, 2020.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news