TFF yafafanua madai ya malipo yaliyomuadhibu Rais wa CAF

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limesema kuwa, Rais wake Wallace Karia hausiki katika malipo yanayodaiwa kusababisha kufungiwa kwa Rais wa Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF), Ahmad Ahmad kwa muda wa miaka mitano juu ya matumizi mabaya ya fedha, anaripoti Mwandishi Diramakini

TFF imetoa taarifa hiyo leo Novemba 24, 2020 ikwa ni siku moja baada ya ya Shirikisho la Soka Ulimwenguni (FIFA) kumfungia Ahmad Ahmad mbaye anatuhumiwa kwa vitendo vya rushwa, ubadhilifu pamoja na matumizi mabaya ya madaraka.Rais wa TFF,Karia.

Awali CAF iliweka wazi kuwa, kiongozi huyo ambaye alikuwa ameshatangaza nia ya kugombea nafasi hiyo kwa kipindi kingine huku nchi 46 zikitangaza kumuunga mkono alikuwa amekiuka majukumu ikiwemo ubadhirifu, kutoa zawadi kwa upendeleo, rushwa na kutumia vibaya madaraka yake ya urais.

Hukumu hiyo ilizua hofu kwa wadau mbalimbali wa soka hapa nchini wakiamini kuwa huenda Tanzania ikakumbana na rungu baada ya kutajwa kupatiwa gawio la kiasi cha dola za Marekani 100,000 ambazo zilielekezwa kugawanywa katika maeneo mbalimbali ikiwemo katika kuendeleza shughuli za soka la vijana.

Miongoni mwa fedha hizo dola 20,000 zilitakiwa kuwekwa kwenye akaunti binafsi za marais wa soka kwa ajili ya posho na kutekeleza majukumu yao, lakini inaelezwa fedha hizo hazikuwekwa bali zote ziliingia kwenye akaunti ya TFF.

Afisa Habari wa TFF, Clifford Ndimbo kupitia taarifa hiyo amesema, itakumbukwa kuwa Mei 2017, Kamati ya Utendaji ya CAF ilipitisha uamuzi kuwa kila mwanachama wake ikiwemo TFF, kupatiwa mgawo wa dola za Marekani 100,000 ambazo ziligawanywa katika katika maeneo mbalimbali.

Jumla ya dola 80,000 zilielekezwa katika matumizi ya shughuli za maendeleo ya Soka la vijana na dola 20,000 zilielekezwa kuingizwa kwenye akaunti kwa Rais wa Shirikisho husika kwa ajili ya kumsaidia katika majukumu yake ya shughuli za mpira wa miguu kutokana na ukweli kuwa hawalipwi mishahara.

Baada ya mgawo huo wa CAF kuingia kwenye akaunti ya TFF, Rais Karia alielekeza fedha hizo dola 20,000 zitumike kwa shughuli mbalimbali za shirikisho kutokana na changamoto ya kifedha iliyokuwepo hivyo hakuna fedha ya CAF iliyowahi kuingizwa kwenye akaunti binafsi ya Rais Karia.

“Chochote ambacho kinaongelewa kwenye mitandao ya kijamii hakina ukweli wowote na jambo zuri ni kuwa Leodigar Tenga ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya CAF na wakati wanapitisha maazimio hayo na kuyapitisha alikuwepo.

“Suala hili tulishalitolea ufafanuzi Aprili, mwaka huu lilipoibuka kwa mara ya kwanza na niwahakikishie fedha zinazotajwa hazikuwahi kulipwa katika akaunti binafsi ya Rais Karia,” imeeleza taarifa hiyo.

Hata hivyo, taarifa ya TFF imesema kuwa, Kamati ya Maadili ya FIFA iliyomfungia Rais Ahmad haikuzungumza chochote kuhusu fedha hizo kwenda kwa marais wa wanachama wa CAF na kuanzia sasa haitasita kuchukua hatua za kisheria dhidi ya wote watakaoendelea kusambaza taarifa hizo za uongo hapa nchini.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news