Vijana wazalendo kufanya kambi ya kuwaleta vijana pamoja

Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali nchini Tanzania wameombwa kuwasaidia vijana katika kambi ya kitaifa ya vijana wazalendo na wapenda maendeleo inayotarajiwa kufanyika Desemba 4 hadi 6,2020 Visiwani Zanzibar ili kuleta tija kwa vijana, anaripoti Mwandishi Diramakini.
Wito huo umetolewa mapema leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi isiyokua ya kiserilaki, National Yourth Camp, Zakayo Shushu, ambapo amesema kambi hiyo ya taifa ya vijana ina lengo kubwa la kuwaleta vijana pamoja ili kujadili namna vijana wapende na kulithamini taifa lao.

"Tumeamua kufanya kambi hii ili kuwajengea vijana uwezo wa kuipenda nchi yao kwa nadharia na vitendo na kutunza rasilimali tulizo nazo ikiwemo rasilimali watu,"amesema Zakayo.

Aidha, amesema kambi hiyo itakayofanyika visiwani Zanzibar kwa siku tatu katika Mikoa mitatu ikiwemo Mkoa wa Kaskazini Unguja, Kusini pamoja na Magharibi ambapo pia wataweza kupatiwa mafunzo na kupewa cheti.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kupinga Vitendo vya Udhalilishaji Zanzibar (ZAFAKH), Chiku Marzouk Ali amesema kuwa, kwa upande wao watashiriki katika kambi hiyo wao kama jumuiya watatoa elimu juu ya masuala ya kujikinga na madhara ya udhalilishaji kwa vijana na kuhakikisha kongamano hilo linafanyika salama.

Naye, Mkurugenzi wa Taasisi ya Malembo Farm, Lucas Malembo amesema kuwa vijana kama nguvu kazi ya taifa wanapaswa kujadiliana kwa pamoja ni jinsi gani wanaweza kushiriki katika kujenga maendeleo ya taifa.

Amesema kuwa, vijana wanachangia kwa kiasi kikubwa katika uchumi wa kati kwa kushiriki katika mambo mbalimbali hivyo ni vyema vijana kuchangamkia fursa hiyo kwa kuweza kujadiliana mambo mbalimbali ya kukuza na kuthamini uzalendo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news