TAMWA yawataka wajasiriamali kuongeza ufanisi

Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA) Zanzibar kimewataka wajasiriamali wanaowasimamia kuhakikisha wanaongeza ufanisi katika uzalishaji wa bidhaa ili ziweze kuwa kivutio kwa lengo la kuongeza kipato kwa manufaa yao,anaripoti Talib Ussi (Zanzibar).

Afisa uwezeshaji kiuchumim TAMWA-Zanzibar, Nairat Abdalla Ali akionesha mfano wa bidhaa ambazo zimehifadhiwa vyema katika mfumo mzima wa vifungashio kwa wajasiriamali.

Akizungumza na wajasiriamali hao Afisa uwezeshaji uchumi Nairat Abdalla Ali katika ukumbi wa chama hicho uliopo Tunguu Wilaya ya Kati Unguja amewataka wajasiriamali hao kutumia fursa wanazopatiwa kila siku zikiwemo za kujengewa uwezo kuwa sehemu ya mabadiliko.

Amesema, kikawaida ili mteja anunue bidhaa anahitaji kuona ubora wa bidhaa hizo na sio kuzalisha bidhaa zisizokua na kiwango ambazo anaamini haziwezi kufanya vizuri sokoni.

Awali afisa masoko kutoka Tamwa-Zanzibar, Muhidini Ramadhan aliwataka wajasiriamali hao kutokata tamaa na changamoto zinazowakabili.
 
Amesema, licha ya kuwepo kwa changamoto mbali mbali wakati wa uzalishaji wa bidhara hizo lakini hawapaswi kuzichukua chanagamoto hizo kuwa sababu ya kukata tamaa na kuacha kuzalisha.

"Sisi TAMWA tunfaham muna chanagmoto nyingi zinazowakabili lakini nawaomba msikate tamaa na zigeuzeni changamoto hizo kuwan sehemu ya fursa,"ameongeza.

Aidha, Afisa huyo wakati akiendelea kufafanua zaidi amesema miongoni mwa njia kuu ambazo zitawafanya wajasiriamali hao kupiga hatua zaidi ni kujenga ushirikiano baina yao na wadau wengine mbalimbali ambao wanaamini watakaua miongoni mwa nyezo za kukuza fursa zaidi ikiwemo kupata masoko.

Kwa nyakati tofauti baadhi ya wajasiriamali hao walisema miongoni mwa changamoto wanazokutana nazo ni upatikanaji wa vifungashio vya bidhaa zao mara wanapomaliza kuzalisha.


Afisa Masoko kutoka TAMWA-Zanzibar, Muhidini Ramadhani akisisitiza jambo kwa wajasiriamali (hawapo pichani) juu ya umuhimu wa kutokata tamaa na kuzalisha bidhaa bora zaidi. (DIRAMAKINI).

Mmoja miongoni mwao, Faida Mohamed Shaibu amesema ni pamoja na uhaba wa masoko ya uuzaji wa bidhaa hizo lakini uhaba wa vifungashio imekua tatizo kubwa kwao.

Amesema, mara nyingi wamewahi kuzalisha bidhaa lakini hukosa kabisa vifungashio ambavyo huhitajika katika utunzaji wa bidhaa hizo kwa mfano chupa na nyenginezo na huelezwa kuwa mzigo haujafika.
 
"Kutokana na mazingira ya aina hii wakati mwengine tunalazimika kubaki na bidhaa zetu majumbani bila ya kuwa na saehemu sahihi ya kuhifadhi na kupelekea kuharibika,’’ameongezea.

Huku hayo yakijiri aliziomba taasisi mbalimbali za kiserikali na watu binafsi kuwekeza nguvu zao katika uzalishaji wa bidhaa za ndani kwa lengo la kuwainua wajasiriamali wa Zanzibar ili waweze kupiga hatua zaidi za kimaendelea na kuliongezea pato taifa kupitia sekta ya kodi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news