Total Tanzania yawashukuru wateja wake

Kampuni ya Mafuta ya Total Tanzania imesema kuwa, wateja wao wamekuwa bega kwa bega katika kuwaunga mkono na bidhaa zao na huduma wanazozitoa hivyo sio wateja bali wamekuwa wadau, anaripoti Mwandishi Diramakini.

Mkurugenzi Mkuu wa Total Tanzania, Jean-Francois Schoepp ameyasema hayo wakati wa awamu ya Pili ya Wiki ya Huduma kwa Wateja katika Kituo cha Mafuta cha Total Africana Mbezi Beach jijini Dar es Salaam.

Amesema kuwa, kutokana na mafanikio makubwa na mrejesho chanya awamu ya kwanza wa wiki maalum ya huduma kwa Wateja ya Total iliyofanyika Novemba 2019 na imeifanya kampuni kurudi tena kwa awamu ya pili katika wiki ya huduma kwa wateja inayolenga kuweka msisitizo wa kujenga mahusiano bora na ya kudumu kwa wateja.

Amesema kuwa, Total kwa mwaka huu imejikita katika katika kutimiza ahadi zake kwa wateja wake wote biashara mtandaoni na Biashara kwenda biashara nyingine (B2C&B2B) kwa kuweka mazingira bora ya kufanya biashara kwa kuwa wasikivu zaidi kwa wateja.

Ni kwa kuandaa hafla maalum zinazowalenga wateja na fursa kwa Total Tanzania kuelezea kwa vitendo kuwa wanawasikiliza na kuwapa kipaumbele wateja.

Schoepp amesema huduma kwa wateja inatoa fursa kwa kampuni kuelewa zaidi changamoto za wateja pamoja na matarajio yao kutoka kwao ili kuweza kuwapatia bidhaa na huduma zitazokidhi mahitaji yao.
 
"Total tunaamini na kutambua kuwa wateja wetu ni zaidi ya wateja na washirika wetu.Wao ndio chanzo cha biashara na mafanikio ya Total nchini, hivyo tunawashukuru sana kwa kuendelea kutuunga mkono na kutuamini na tunawakaribisha wote kutupa mawazo na maoni yenu juu ya huduma zetu tupate kuboresha na kuwapa huduma bora zaidi," amesema Schoepp.

Aidha, amesema kuwa awamu ya pili ya wateja ya Total imekuwa ya mafanikio sana kutokana na jitihada za wafanyakazi wa Total hivyo wataendelea kuwa pamoja na wateja.
Mkurugenzi Mkuu wa Total Tanzania, Jean-Francois Schoepp akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na awamu ya pili ya Wiki ya Huduma kwa Wateja ya Total iliyoanza Novemba 16 na kumalizika Novemba 20 katika Kituo cha Mafuta cha Total Africana Mbezi Beach jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mkuu wa Total Tanzania Jean-Francois Schoepp akiwa na bidhaa ya Kilainishi Cha magari katika Duka la Kituo Cha Mafuta cha Africana Mbezi Beach ambayo Duka la bidhaa mbalimbali vikiwemo na vinjwaji baridi.

Mkurugenzi Mkuu wa Total Tanzania Jean-Francois Schoepp akimhudumia mteja kwa kutumia kadi wakati wa awamu ya Pili ya wiki ya Huduma kwa Wateja wa Total.

Mkurugenzi Mkuu wa Total Tanzania Jean-Francois Schoepp akitoa huduma kwa kuangalia Oil katika gari ikiwa ni awamu ya pili ya wiki ya Huduma kwa Wateja wa Total.

Wafanyakazi wa Total wakiwa katika duka ambalo wanatoa huduma zisizo za Mafuta.

Meneja wa Maduka na Biashara zisizo za Mafuta wa Total Tanzania, Jane Mwita akizungumza huduma zinazopatikana katika Maduka ya vituo vya Mafuta ya Total katika kurahisisha huduma kwa wateja.

Wafanyakazi wa Total Tanzania wakiwa na Mkurugenzi Mkuu mara baada ya kuzindua huduma kwa wateja katika Kituo Cha Mafuta Cha Africana Mbezi Beach jijini Dar es Salaam.

Wafanyakazi wa Total wakifurahi jambo mara baada ya kuzindua.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news