TPDC yang'ara mashindano ya SHIMUTA

Timu ya Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini (TPDC) wameibuka na ushindi wa seti 2-0 katika mchezo wa kuvuta kamba dhidi ya timu ya Shirika la Viwango Tanzania (TBS) katika muendelezo wa michuano ya Shimuta inayoendelea jijini Tanga, anaripoti Mwandishi Diramakini. 
Awali wanaume walivuta kamba na Chuo cha DIT na kupata seti 2-0 na leo wamevuta na chuo cha IAA na kupata mivuto 2-0 na wanaamini mechi zilizobaki wataendelea kushinda na kutinga hatua ya fainali. 

Mchezo huo huo uliochezwa kwenye uwanja wa Shule ya Sekondari Popatlal Jijini Tanga leo ulionekana kuwa na upinzani, lakini TPDC ambao walikuwa wamesheheni wachezaji mahiri na wenye viwango waliweza kuwagaragaza wapinzani wao. 

Akizungumzia ushindi huo na namna walivyojipanga kuelekea kwenye michezo yao mingine,Kocha wa timu hiyo, Joram Ndalalwa amesema timu hiyo imejipanga vizuri kunyakua ubingwa kwenye michuano hiyo. Joram amesema kila wakati mara baada ya kumalizika kwa mchezo mmoja wanarudi kujitafakari na kujipanga upya kuona namna ya kujiandaa vema.

Amesema baada ya kumalizika mchezo huo na kuweza kuibuka na ushindi wanarudi kujipanga kwa ajili ya mchezo wao unaofuata dhidi ya ATC na baadae UDSM. 
Akizungumzia mashindano hayo Katibu wa Michezo kutoka TPDC ,Elinaike Naburi amesema kwamba walishiriki mashindano hayo ya Shimuta mwaka huu ikiwa ni mara yao ya tano mpaka sasa wamekwisha kushiriki michezo wa mpira wa miguu,wavu,pete,kikapu pamoja na michezo ya Jadi,Karata,Table na Draft. 

Amesema mchezo wa vishale watamaliza kuanzia Novemba 24 na 25 watafanya mbio mpaka sasa wamefanikiwa kutinga hatua ya 16 katika mpira wa miguu na Pete waliishia kwenye makundi kwa kuwa mshindi wa tatu huku Wavu wakiishia kwenye makundi, lakini walionyesha ushindani mkubwa. 

Kikapu waliishia kwenye makundi lakini ushindano wao ulikuwa wa hali ya juu katika michezo ya jadi wameshinda kwa kuwa mabingwa karata upande wa wanawake na mshindi wa pili upande wa wanaume. Katika mchezo wa drafti alisema waliishia hatua ya robo fainali upande wa wanaume huku wanawake wakiishia hatua za makundi na mchezo wa Pooltable wanawake wamefanikiwa kutetea taji lao kwa kuwa mshindi wa pili mwaka jana mshindi wa kwanza na wanaume waliishia nusu fainali.

Amesema kwamba, katika mchezo wa bao wachezaji wao wote wameishia hatua ya nusu fainali huku akieleza malengo ya mashindano hayo kwa TPDC ni kuonyesha ushindani wa hali ya juu. 

Katibu wa Michezo kutoka Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC), Elinaike Naburi akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kwenye viwanja vya shule ya Sekondari Popatlaly kuhusu namna timu zao zilivyofanya vizuri katika mashindano ya SHIMUTA.

Amesema pia malengo yao ni kuweza kufahamiana na taasisi nyingine kujenga mshikamano kama wafanyakazi na kuendelea kutoa morali na motisha kwa wafanyakazi kuendelea kushiriki michezo kwa sababu ni afya. 

Hata hivyo amesema wamefurahi kupata nafasi ya kushiriki mashindano hayo na wanaamini wametoa ushindani wa kutosha na wataendelea kufanya hivyo michezo yao iliyobaki.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news