Hakimu Mfawidhi ahukumiwa miaka mitatu jela

Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Babati mkoani Manyara, I.B Kuppa amemuhukumu kwenda jela miaka mitatu au kulipa faini ya sh. milioni 1, 500,000 aliyekuwa Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Mwanzo ya Magugu, Adeltus Richrad Rweyendera, anaripoti Mwandishi Diramakini.

Rweyendera amepewa adhabu hiyo katika kesi ya rushwa Namba CC.137/2020 baada ya kupatikana na hatia ya makosa ya kuomba na kupokea rushwa ya shilingi 150,000 kinyume na kifungu cha 15 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa na 11, 2007.

Rweyendera aliomba fedha hizo toka kwa wazazi wa ndugu wa washitakiwa watatu ambao walikuwa wanashtakiwa kwenye kesi Namba 242/ 2020 ikiwa ni kishawishi cha kuwasaidia na kuwaachia washitakiwa hao kwenye kesi tajwa ambayo hakimu huyo alikuwa anaisikiliza katika Mahakama ya Mwanzo Magugu.

Hukumu hiyo ilitolewa na Mheshimiwa I.B Kuppa baada ya waendesha mashtaka wa TAKUKURU, Martin Makani na Evelyne Onditi kuwasilisha ushaidi usioacha shaka dhidi ya mshtakiwa Rwenyendera kwa mujibu wa Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya jinai mwaka 1985, hivyo Mahakama ikamkuta na hatia na kutoa adhabu kwa mujibu wa sheria.Post a Comment

0 Comments