Mbunge Sagini atatua kero za wananchi papo kwa papo Butiama

Mbunge wa Jimbo la Butiama mkoani Mara, Jumanne Sagini amepiga kambi jimboni humo kuhakikisha anasikiliza, wanashirikishana na kuzitatua kero zinazowakabili wananchi wake papo kwa papo, anaripoti Mwandishi Diramakini (Butiama).
Katika ziara hiyo ambayo imepongezwa na wananchi licha ya kushiriki katika shughuli za maendeleo ya kijamii pia amechangia mifuko ya saruji zaidi ya 255 kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya shule.

Wakati huo huo, Mheshimiwa Sagini ameonyesha kutofurahishwa na hali ya kutokamilika kwa ujenzi wa jengo la Halmashauri ya Wilaya ya Butiama huku akiiomba Serikali iingilie kati.

Mheshimiwa Mbunge wa Jimbo la Butiama yuko jimboni kwake Butiama kwa muda akifanya ziara kwa kusikiliza kero za wananchi,kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo na amejiwekea utaratibu wa kuzunguka na Mkurugenzi 

Mtendaji Butiama na hii imemsaidia kero zingine za wananchi kuzitatua hapo hapo kupitia ziara hiyo.Pia Mheshimiwa Mbunge Jumanne Sagini ametembea kata za Buswahili, Sirorisimba, Busegwe, Butiama, Kyanyari, 

Kamugegi na Nyamimange katika ziara hiyo amechangia saruji mifuko 255 katika kata hizo.Aidha, amegawa mipira zaidi ya 40 kwa vijana kwa ajili ya michezo,kusaidia vikundi vya vijana kata ya Nyamimange, na ametoa fedha taslimu zaidi ya sh.milioni tano katika sekta ya elimu na kilimo kwa kuvinunulia vikundi mbegu bora za mihogo vikundi zaidi ya 15 ili kuhakikisha wanapata mbegu bora za kuweza kuwasaidia kupata zao bora la chakula na biashara.
Wakati huo huo Mheshimiwa Mbunge wa Jimbo la Butiama ameiomba Serikali kumaliza ujenzi wa jengo la Halmashauri ya Butiama, kwani hadi sasa lipo katika hali mbaya.

"Naiomba Serikali iweze kutusaidia kumaliza ujenzi huu ili watumishi wetu na wananchi waweze kupata huduma bora, jengo tunalotumia sasa tunajibana idara zaidi ya moja katika ofisi moja ni shida,"amesema Mbunge Sagini.
Mbunge wa jimbo la Butiama anaendelea na ziara yake katika jimbo la Butiama ili kuhamasisha jamii katika shughuli za maendeleo, kusikiliza kero na kuzipatia majawabu.

Wakati huo huo, Mheshimiwa Sagini katika kuasaidia ujenzi amesaidia Jeshi la Magereza Kiabakari saruji mifuko 40 ili waweze kuboresha miundombinu yake.
Mbunge wa Jimbo la Butiama mkoani Mara, Mheshimiwa Jumanne Sagini katika picha tofauti akionekana kushiriki shughuli mbalimbali za kijamii jimboni humo ikiwa ni mwendelezo wa ziara zake mfululizo kwa ajili ya kusikiliza kero za wananchi na kuzipatia ufumbuzi jimboni humo. (Picha zote na Mwandishi Diramakini).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news