KIONGOZI MWANDAMIZI WA KMC FC AFARIKI

Kiongozi Mwandamizi wa Timu ya KMC FC ndugu, Raphael Waryana amefariki dunia asubuhi ya leo katika hospitali ya Taifa Muhimbili baada ya kuugua kwa muda mfupi.
Ndugu Waryana atakumbukwa kwa mchango wake mkubwa ambao alikuwa akiutoa katika Timu ya KMC FC ikiwa ni pamoja na ushirikiano wake katika kipindi ambacho Timu ilipokuwa ikitimiza majukumu yake.

Aidha, uongozi umeshtushwa na taarifa hiyo na kuahidi kuendelea kuuenzi mchango wake mkubwa aliokuwa anautoa kwa Timu wakati wa uhai wake.

Uongozi unatoa pole kwa familia yake, mashabiki wa Timu ya KMC FC na Umma wa wanamichezo na kuwaomba wawe na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha kumpoteza mpendwa wetu.

Imetolewa na Christina Mwagala

Afisa Habari na Mahusiano wa Timu ya KMC FC

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news