Maelfu ya Watanzania wanatarajiwa kukusanyika katika Huduma ya Sauti ya Uponyaji iliyopo Yespa, Kihonda mjini Morogoro kwa ajili ya kuliombea Taifa na viongozi wake,anaripoti Mwandishi Diramakini.
Ibada hiyo itaenda sambamba na maombi kwa viongozi wote wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakiongozwa na Rais Dkt.John Magufuli akiwemo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt.Hussein Ali Mwinyi.

Kiongozi Mkuu wa Huduma ya Sauti ya Uponyaji Tanzania, Nabii Joshua Aram Mwantyala akiwa katika maombi maalum ya kuliombea Taifa ndani ya mlima wa maombi. (Picha na SUT).
Kiongozi Mkuu wa Huduma ya Sauti ya Uponyaji Tanzania, Nabii Joshua Aram Mwantyala ameyasema hayo leo Februari 1, 2021 wakati akiendelea na maombi mfululizo kwa ajili ya kuliombea Taifa ili Mungu aweze kulivusha katika vikwazo na changamoto mbalimbali. Huku wakiongozwa na neno la Mungu kutoka 1 Wathesalonike 5:17, Biblia inaeleza kuwa, "ombeni bila kukoma".
Nabii Joshua amesema kuwa, huu ni wakati wa kujinyenyekeza mbele za Mungu kwa kuwa, kila amtegemeaye Mungu huyashinda mambo yote. "Tarehe 6 na 7, Februari,mwaka huu, hasira ya Bwana itawaka juu ya watesi wako, hivyo kwa pamoja tufike, Mungu akatutendee mema,"alisema.

Wakati huo huo, Nabii Joshua amewaomba wakuu wetu wa nchi kuendelea kumtegemea Mungu kwa kila jambo wanalotaka kulifanya katika Taifa letu kwa kuwa, moyo huo unaenda kuwashangaza maadui wengi ambao wanainenea mabaya Tanzania.
Amesema, anaendelea na mfululizo wa maombi ya kuwakabidhi viongozi hao, wasaidizi wao na Watanzania mbele za Mungu ili Mungu aweze kuwashindia changamoto na majaribu mbalimbali ambayo wanapitia.
"Katika kitabu cha Yeremia 33:3, Biblia inasema, niite, nami nitakuitikia, nami nitakuonyesha mambo makubwa, magumu usiyoyajua.
"Maneno haya ni Mungu aliyazungumza kwa kinywa cha Yeremia, alipokuwa katika gereza alilokuwa amefungwa, wakati huo Mji wa Yerusalemu ulikuwa umeshazungukwa na majeshi ya Nebukadneza na ndani ya mji kuna njaa kali.
"Lakini kama Biblia inavyosema katika kitabu cha Maombolezo 3:31,Mungu hatamtupa mtu hata milele. Maana yake ni kwamba kutakapotokea mitikisiko hata mtu akageuka na kumwacha Mungu na mtu yule akaadhibiwa katika dhambi zake, na mtu yule akatubu mbele za Mungu.
"Basi Mungu hataishikilia adhabu yake juu ya huyo mtu milele.Itafika kipindi atamrehemu tu, hivyo ninaamini licha ya changamoto tunazopitia kwa sasa ikiwemo kunenewa mambo mabaya na maadui kutoka ndani na nje ya nchi, bado Mungu wetu anatupenda na ushindi tunakwenda kuupata,"amesema.

Tags
Habari