Rais Magufuli ampangia aliyekuwa Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam Sipora Liana kuwa Mkurugenzi Manispaa ya Kinondoni

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.John Pombe Joseph Magufuli amempangia kazi Bi.Sipora J. Liana kuwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni kuanzia leo Februari 25, 2021, anaripoti Mwandishi Diramakini.

Taarifa iliyotolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo imesema Bi. Sipora Liana amepangiwa majukumu hayo baada ya lililokuwa Jiji la Dar es salaam kuvunjwa hapo jana Februari 24,2021.
Bi.Sipora Liana

Waziri Jafo alieleza kuwa utaratibu wa kuwahamisha wafanyakazi katika vituo vingine utaendelea.

Aidha Waziri Jafo amemkabidhi Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es salaam Mhe.Omary Kumbilamoto (aliyekuwa Mstahiki Meya wa Ilala) Gari lililokua likitumiwa na Mstahiki Meya wa Jiji lililovunjwa la Dar es Salaam.

Post a Comment

0 Comments