Tanzania yatoa msimamo kuhusu chanjo ya Corona

Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imesema haina mpango wa kupokea chanjo ya virusi vya Coroa (COVID-19) inayoripotiwa kuwepo na kutumika kwenye mataifa mengine, anaripoti Mwandishi Diramakini.
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.Dorothy Gwajima. (Picha na Maktaba).

Hayo yamebainishwa na Waziri wa wizara hiyo, Dkt. Doroth Gwajima wakati akitolea ufafanuzi maswali mengi ambayo yamekuwa yakiulizwa na waandishi wa habari iwapo wizara ina mpango wa kupokea chanjo ya virusi hivyo na njia zipi zitumike kujikinga na ugonjwa huo.

Dkt.Gwajima amesema kuwa,Serikali kupitia Wizara ya Afya inazo taratibu zake za kufuata pale inapotaka kupokea bidhaa yoyote ya afya na hufanyika baada ya Serikali kujiridhisha.

"Hivyo hadi tujiridhishe na siyo vinginevyo,"amesema huku akiweka wazi kuwa, kuhusu mbinu za kujikinga na ugonjwa huo,wizara inaendelea kuwakumbusha wananchi kujielekeza kwenye elimu ambayo imekuwa kitolewa na wataalamu wa afya ikiwemo kuimarisha usafi.

Amesema,wizara kwa ushinkiano na Mkemia Mkuu wa Serikali na Baraza la Tiba Asili, wananchi, wajuzi wa Tiba Asili tayari wameshafanya uchunguzi dawa za tiba asili.

Miongoni mwao dawa ya COVID-19 ambayo imekuwa inawasaidia wagonjwa wanaougua magonjwa mbalimbali ikiwemo haya ya mfumo wa hewa ni pamoja na dawa ya COVIDOL ambayo imekuwa ikiwasaidia sana wagonjwa wanaougua magonjwa mbalimbali yakiwemo ya mfumo wa hewa, huku akitaja dawa za NIMRCAF,PLANET++,BINGWA na COVOTANXA ambazo amesema zinakamilisha taratbu za matumizi.

Amesema, uko ushahidi wa kutosha kabisa kuhusu watu wengi ambao wamepata ugonjwa huo na kupona magonjwa mbalimbali ya kuambukiza na yasiyoambukiza yaliyokuwa yanawasumbua mara baada ya kutumia dawa za tiba-asili hata kama walikuwa kwenye matibabu mengine ya dawa za hospitali.

Dkt.Gwajima amesema elimu ya kujikinga na magonjwa ya kuambukiza na yasiyo ya kuambukiza pamoja na matumizi ya tibaasili itaendelea kutolewa na wataalam wa afya .

Pia ametumia nafasi hiyo kulielekeza Baraza la Tiba Asili kutoa orodha ya dawa zote ambazo zimepita kwenye utaratibu wa kufanyiwa uchunguzi wa kimaabara na maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali na kuonekana kuwa matokeo ya awali ya uchunguzi ni salama kwa matumizi na kwa kuwa dawa hizo zimekuwa zikitumiwa na watu wengi na kuwaponya ama kuwapatia nafuu,jamii ifahamu uwepo wake,gharama pamoja na zikopatikana.

Dkt.Gwajima amesema, Serikai itaendelea kuchukua tahadhari zote za ufuatiliaji wa mwenendo wa magonjwa yote kama ambavyo imekuwa ikifanya siku zote na kuendelea kuelimisha wananchi juu ya hatua za kuchukua.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here