AKIBA COMMERCIAL BENKI YAINGIA MAKUBALIANO YA UBIA WA KIMKAKATI NA BENKI YA BIASHARA MALAWI

Banki ya Akiba Commercial (ACB Pls) imeingia makubaliano ya ubia wa kimkakati na Benki ya Biashara ya Malawi ambayo imewekeza mtaji wa sh.Bilioni 17 ili kuimarisha utendakazi wa benki hiyo, anaripoti Mwandishi DIRAMAKINI (Dar es Salaam).

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Akiba Commercial Benki Juliana Swai (kulia) akizungumza na wanahabari wakati wa hafla ya kutangaza kuwa Benki ya Akiba imepata mbia wa kimkakati yaani strategic investor ambaye ni National Bank of Malawi Kupitia mbia huyo Benki ya Akiba sasa inaweza kuimarisha mtaji wake na kukidhii vigezo vya Benki Kuu kuhusiana na swala zima la mtaji, hafla hiyo imefanyika leo makao makuu ya benki hiyo iliyopo mtaa wa Ohio jijini Dar es Salaam kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa benki hiyo Dora Saria. (Picha na Mwandishi DIRAMAKINI).
 
Hayo yamesemwa leo Machi 3, 2021 jijini Dar es Salaam na Kaimu Mkurugenzi wa Mtendaji wa Benki ya Akiba, Juliana Swai wakati akizungumza na waandishi wa habari.

"Akiba Commercial Bank ni Benki ya kibiashara ambayo tangu kuanzishwa kwake mnamo mwaka 1997 imekuwa ikitoa huduma zake kwa wateja wengi wakiwa ni wajasiriamali wadogo,wakati na wa juu yaani Micro, Small and Medium entrepreneurs (MSMEs). 

"Benki imeweza kuwafikia zaidi ya Watanzania 200,000 katika mikoa ya Dar es Salaam, Arusha, Mwanza, Mbeya, Kilimanjaro, na pamoja na Makao makuu ya nchi Dodoma. Watanzania hawa wameweza kufaidika na huduma za mikopo mbalimbali ya kijasiriamali pamoja na amana za aina zote kuanzia watoto wadogo, vijana na watu wazima.

Aidha, huduma za benki kupitia simu za mikononi yaani Akiba Mobile zimeleta unafuu na urahisi zaidi katika kuwafikia wateja popote pale walipo. Baada ya utangulizi huo ningependa sasa kutoa taarifa rasmi kuhusiana na mikakati mbalimbali ya kimaendeleo ndani ya Benki ya Akiba ambayo itapelekea kuleta mabadiliko makubwa katika tasnia ya kifedha,"amefafanua Kaimu Mkurugenzi Mtendaji huyo.
 
Amesema, Benki ya Akiba imepata mbia wa kimkakati yaani strategic Investor ambaye ni National Bank of Malawi.
 
Kupitia mbia huyu Benki ya Akiba sasa imeweza kuimarisha mtaji wake na kukidhi vizuri vigezo vya Benki Kuu kuhusia na na suala zima la mtaji wa uendeshaji wa Benki ya Kibiashara baada ya mbia wake NBM kuweka kiasi cha shilingi za Kitanzania zipatazo bilioni 17.
 
"Lengo kuu la mkakati huu ni kuimarisha mtaji wa benki kama nilivyosema hivi punde. Lakini pia benki imekuwa ikiangalia mahitaji ya soko lake na kuona kuwa kuna haja ya kupata mwekezaji au mbia wa kimkakati kwa ajili ya kuifanya benki iwe imara zaidi na kuweza kuboresha huduma zake na kuanzisha huduma nyingi zaidi ambazo zinahitajika kwenye soko la Kitanzania,"amesema.
 
Amesema, kupitia ubia huu naomba niwaahidi wateja wetu na Watanzania wote kwa ujumla mabadiliko makubawa na chanya katika huduma zetu na mifumo yetu ya utoaji huduma.
 
"Tunaamini kuwa tutaweza kuwahudumia wateja wetu kwa weledi zaidi kupitia utalaamu na uzoefu wa taasisi mbili hizi bobezi kwenye sekta ya fedha. Pia, tunatambua mahusiano mazuri na undugu kati ya nchi hizi mbili na ambazo pia zina mahusiano makubwa ya kibiashara.
 
"Faida moja wapo ya wazi ni kuwepo kwa mazingira wezeshi ya kufanya biashara kati ya nchi hizi mbili kupitia huduma za kifedha ambazo zitapatikana kwa urahisi zaidi. Aidha, uwekezaji huumutausaidia pia kuwepo kwa mazingira wezeshi ya ufanyajibiashara kwa nchi ambazo zipo kusini mwa Bara la Afrika wakiwepo wanachama wa SADC,"amefafanua Bi.Swai.
 
Ameongeza kuwa, Malawi ni moja ya nchi zilizopo Kusini mwa Afrika zinazotumia Bandari ya Dar es Salaam kama lango kuu la kibiashara. 
 
“NBM ambayo ilianzishwa mwaka 1971 baada ya muungano wa Barclays Bank DCO na Benki ya Standard ya Afrika Kusini, ni moja ya benki kubwa nchini Malawi inayotoa huduma za benki ikiwemo rejareja yaani Personal and Retail banking, wateja wakubwa, huduma za kibenki za uwekezaji na udalali katika soko la hisa na mitaji.
 
“Kwa sasa Akiba Commercial Benki imekuwa mhimili imara katika sekta ya fedha na imefungua ukurasa mpya kibiashara. Nawakaribisha Watanzania wote wafike Akiba Commercial Bank ili waweze kufaidika na fursa mbalimbali kwa maendeleo ya maisha yao na biashara zao. Akiba Commercial Bank, benki kwa maendeleo yako,”amefafanua Bi.Swai.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news