Kocha wa Yanga, wenzake wafutwa kazi wakijiandaa kurejea Dar


Sare ya kufungana bao 1-1 kati ya Yanga SC dhidi ya Polisi Tanzania, imesababisha uongozi wa Yanga kutangaza kuvunja benchi la ufundi lililokuwa likiongozwa na Kocha Mkuu, Cedric Kaze raia wa Burundi.

"Hatuna la kusema, nasi hizi taarifa zimetushtua sana ila hayo ndiyo maamuzi ya uongozi. Tumefanya kila linalowezekana kuhakikisha tunaiweka klabu katika hali nzuri, lakini haikuwa bahati, tutasema zaidi wakati ujao," Mwandishi DIRAMAKINI amemnukuu mmoja kati ya viongozi hao waliofutwa kazi.

Post a Comment

0 Comments