Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (Mb) Balozi Liberata Mulamula akiwa katika mazungumzo na Balozi wa Israel hapa Nchini Balozi Oded Joseph mazungumzo yaliyofanyika katika Ofisi za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dodoma. Katika mazungumzo hayo Balozi Mulamula amemsihi Balozi Oded kuhakikisha Israel inakuwa na Ubalozi wake rasmi hapa Nchini na kumshukuru kwa hatua ya Israel kuwachukuwa vijana wa Kitanzania kwenda Nchini humo kwa mafunzo ya vitendo na nadharia kuhusu kilimo.Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (Mb) Balozi Liberata Mulamula akiwa katika mazungumzo na Balozi Regina Hess mazungumzo hayo yamefanyika katika Ofisi za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dodoma. Pamoja na masuala mengine Viongozi hao walijadili masuala ya ushirikiano katika sekta ya afya,elimu,biashara,uwekezaji pamoja na maliasili na utalii.
Tags
Picha