Yanga SC yatoshana nguvu na KMC FC kwa bao 1-1

Klabu ya Yanga imeendelea kushusha matumaini ya ubingwa baada ya kulazimishwa sare ya 1-1 na KMC FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara.

Ni kupitia mtanange uliochezwa leo majira ya saa 1 usiku katika simba la Benjamin Mkapa lililopo Manispaa ya Temeke, Dar sa Salam.

Kino Boy wametangulia kwa bao la Bryson David dakika ya 29, kabla ya Mburkina Fasso, Yacouba Sogne kuisawazishia Yanga SC dakika ya 46.
Aidha, kwa matokeo hayo, Yanga SC inafikisha alama 51 baada ya kucheza mechi 24 na kuendelea kuongoza Ligi Kuu kwa alama nne zaidi ya Azam FC ambayo hata hivyo imecheza mechi moja zaidi.

Hata hivyo, mabingwa watetezi, Simba wanashika nafasi ya tatu wakiwa na alama 46 baada ya kucheza mechi 20.

Awali Dodoma Jiji FC imewachapa wenyeji, Tanzania Prisons 1-0, bao pekee la Dickson Ambundo dakika ya 55 Uwanja wa Samora, Sumbawanga mkoani Rukwa.

Pia Gwambina FC imeitandika Coastal Union 4-0, mabao ya Meshack Abraham dakika ya tisa, Paul Nonga dakika ya 31, Rajab Athumani dakika ya 37 na Jimson Mwanuke dakika ya 75 Uwanja wa Gwambina, Misungwi mkoani Mwanza.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news