Rais Samia kufanya ziara nchini Uganda kushuhudia utiaji saini Mkataba wa EACOP

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kesho April 11,2021 atafanya ziara ya kikazi ya siku moja nchini Uganda kwa mwaliko wa Rais Yoweri Museveni.
Baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Entebbe, Rais Samia atafanya mazungumzo ya faragha na Museveni na kisha Viongozi hao watahudhuria hafla na kushuhudia utiaji saini wa mkataba kati ya Serikali ya Uganda na Kampuni ya Mafuta Ghafi ya Afrika Mashariki (EACOP) juu ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta ghafi la kutoka Hoima, Uganda hadi Tanga, Tanzania.
Hafla ya utiaji saini mkataba huo itafanyika Ikulu Mjini Entebbe na kuhudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Nchi zote mbili na Kampuni zitakazotekeleza ujenzi wa mradi huo mkubwa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news