🔴𝐋𝐈𝐕𝐄:Simba SC vs Gwambina FC leo Aprili 24,2021 WACHEZAJI WAAHIDIWA KUJAZWA FEDHA

Hata hivyo, kwenye mchezo huu wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Simba, uongozi wa Gwambina FC umewatengea mkwanja wachezaji wake ili waifunge Simba leo.

Mtanange huu unapigwa Uwanja wa Gwambina Complex uliopo Misungwi, Mwanza, ambapo kwenye mchezo wa kwanza Gwambina ilikubali kichapo cha mabao 3-0.

Mabao hayo zama za Sven Vandenbroeck wa Simba,yalifungwa na Meddie Kagere, Pascal Wawa na Chris Mugalu kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Championi Jumamosi, Kocha Mkuu wa Gwambina, Mohamed Badru alisema kuwa: “Wachezaji wote wapo fiti kuelekea kwenye mchezo wa kesho (leo) dhidi ya Simba.

Tunafahamu kuwa tunaenda kukutana na timu kubwa yenye ushindani lakini tutapambana ili kuhakikisha tunapata ushindi kwenye uwanja wetu wa nyumbani.

Kwenye michezo miwili iliyopita tumepoteza lakini kadri timu inavyocheza kila siku naona kuna maendeleo makubwa na makosa yanapungua.

“Kuna kiasi cha bonasi kwa wachezaji kimewekwa na uongozi kwa ajili ya kuongeza morali ya wachezaji kupambana ili timu ibaki ligi kuu," amekaririwa Kocha.

Gwambina inashika nafasi ya 12 kwenye msimamo wa ligi baada ya kukusanya pointi 30 ikiwa imecheza mechi 25.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news