TIMU ZA TPDC ZINAZOSHIRIKI MICHEZO YA MEI MOSI MWANZA ZATEMBELEA KITUO CHA WATOTO YATIMA NA KUTOA MISAADA

Watumishi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania-TPDC wanaoshiriki katika michezo mbalimbali kama vile mpira wa miguu, kuvuta kamba,karata, bao pamoja na mpira wa pete kwa ajili ya kuadhimisha siku ya wafanyakazi duniani maarufu Mei Mosi inayofanyika kitaifa jijini Mwanza wametembelea kituo cha watoto wanaoishi katika mazingira magumu cha Hisani na kutoa msaada wa vifaa mbalimbali, anaripoti Mwandishi DIRAMAKINI (Mwanza).

Akizungumza leo Aprili 26, 2021 kwa niaba ya timu kiongozi wa timu,Elinaike Naburi alisema kwamba, "TPDC ni Shirika la Mafuta la Taifa na moja kati ya mashirika ya umma yanayoshiriki katika michezo ya Mei Mosi ambayo hufanyika kila mwaka, hivyo mwaka huu tumeona kuna haja pia ya kufanya kitu cha ziada kwa ajili ya kupeleka tabasamu kwa watoto, lakini pia kwa jamii na wadau ambao wanapambana usiku na mchana kulea watoto hawa".

Ameongeza kuwa, "TPDC ni Shirika la watanzania na si mara ya kwanza kwa TPDC kutoa CSR za kuchangia miradi ya kijamii na kimaendeleo, kwani imekuwa ikifanya hivyo katika mikoa mbalimbali ambayo shirika linatekeleza shughuli zake na hata kule ambapo shirika halina mradi wowote,"ameongeza.

Naburi ameongeza kuwa, watoto hao hawakutamani kuzaliwa wajikute katika mazingira hayo, "bali ni changamoto mbalimbali za kimaisha ambazo zimewafanya wakajikuta katika mazingira haya,hivyo ni rai yangu kwa wadau wengine wa maendeleo kujitoa kusaidia watoto hawa ili nao waweze kutimiza ndoto na malengo yao na baadae kulisaidia taifa kwa ujumla,"aliongeza.

Kwa upande wake Msimamizi wa Kituo cha Hisani, Grace Peter alishukuru kwa msaada huo ambapo alisema wana jumla ya watoto 105 wavulana wakiwa 96 huku wasichana wakiwa 9 na wote wanasoma.

Grace metoa wito kwa wadau mbalimbali kujitoa kwa ajili ya kusaidia watoto hao katika mahitaji mbalimbali.

Vifaa vilivyopelekwa na TPDC na kupokelelewa kituoni hapo ni pamoja na unga wa mshindi kilo 25, sukari kilo 25,sabuni za kufulia za miche katoni sita,chumvi dazeni moja, dawa ya meno katoni mbili, mafuta ya kula ndoo mbili na mafuta ya kujipaka katoni nne.

Baadhi ya wawakilishi wa timu za michezo za Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini (TPDC) wakikabidhi vifaa mbalimbali kwa kituo cha kuhudumia watoto yatima cha Hisani kilichopo jijini Mwanza.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news