Frank Mwita mbaroni kwa kukutwa na kilo 446.11 za bangi

Mfanyabiashara, Frank Mwita anayeishi mkoani Dar es Salaam amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu iliyopo jijini Dar es Salaam akikabiliwa na shitaka la kukutwa na zaidi ya kilo 446.11 za dawa za kulevya aina ya bangi.
Katika hati ya mashtaka iliyosomwa mahakamani hapo na wakili wa serikali Mwandamizi, Wankyo Simon mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Augustina Mmbando imedai, Februari 25, mwaka huu huko katika Kijiji cha Wavuvi Kurasini ndani ya Manispaa ya Temeke mkoani Dar es Salaam mshtakiwa alikutwa akiwa na kilo 446.11 za dawa za kulevya aina ya bangi.

Aidha, mshtakiwa hakuruhusiwa kujibu kitu chochote mahakamani hapo kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za dawa za kulevya. 

Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika na kesi hiyo imeahirishwa hadi Juni 3, 2021 itakapokuja kwa ajili ya kutajwa na mshtakiwa amerudishwa rumande.

Post a Comment

0 Comments