Profesa Mdoe awakaribisha Watanzania kujifunza mbinu bora za kilimo Banda la TARI mkoani Dodoma

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, Prof. James E Mdoe, amewataka wananchi jijini Dodoma kuendelea kutembelea banda la Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) ili kuweza kupata elimu juu ya kilimo bora cha mazao mbalimbali yanayoratibiwa na vituo vyote vya TARI nchini.

Prof.Mdoe ameyesema hayo alipotembelea banda la TARI ili kuoneshwa na kujifunza teknolojia mbalimbali zinazozalishwa na watafiti.

Katika banda la TARI pia ametembelea Balozi wa Sweden nchini, John Hellstrom aliyeambatana na Mkurugenzi Mkuu wa Costec ambaye pia ni mjumbe wa bodi ya TARI, Dkt. Amos Nungu. (Picha zote na TARI).

Post a Comment

0 Comments