MCHEZAJI WA KLABU YA EINTRACHT FRANKFURT AENDELEA KULA BATA SERENGETI

Mchezaji soka la kulipwa nchini Ujerumani na mzaliwa wa Mali, Almamy Toure anatembelea Hifadhi ya Taifa ya Serengeti mkoani Mara kwa lengo la kutalii na kufurahia mapumziko yake.
Almamy Touré ambaye anachezaji kama mlinzi wa kulia katika ligi ya Bundesliga kwenye klabu yake ya Eintracht Frankfurt kwa sasa anaiwakilisha Ufaransa kimataifa.

Katika msimu huu uliomalizika mwezi uliopita, timu ya mchezaji huyo Eintracht Frankfurt imeshika nafasi ya tano na katika ukurasa wake wa Facebook aliandika masikitiko yake kwa kumaliza ligi vibaya huku akishindwa kuisaidia kutokana na kuwa majeruhi.

Post a Comment

0 Comments