Rais Samia afanya uteuzi leo Juni 8, 2021

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amemteua Prof. Eleuther Alphonce Mwageni kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE).

Prof. Mwageni ni Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU) na anachukua nafasi ya Prof. Esther Ishengoma ambaye amemaliza muda wake.

Gerson Msigwa ambaye ni Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu ameeleza kupitia taarifa yake leo Juni 8, 2021 kuwa,uteuzi huu umeanza jana tarehe 07 Juni, 2021.
Wakati huo huo, Mhe. Rais Samia amemteua Dkt. Neema Bhoke Mwita kuwa Mjumbe wa Baraza la Ushindani (Fair Competition Tribunal).

Dkt. Mwita amechukua nafasi ya Dkt. Theodora Nemboyao Mwenegoha ambaye ameteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania.Uteuzi huu umeanza leo tarehe 08 Juni, 2021.

Post a Comment

0 Comments