Magazeti leo Aprili 12,2026

Tanzania imeendelea kung’ara katika anga la kimataifa baada ya kuingiza vipengele 41 katika Tuzo za Utalii na Usafirishaji Duniani (World Travel Awards), hatua inayoimarisha nafasi yake kama moja ya vinara wa utalii barani Afrika.
Akizungumza, Aprili 11,2026 jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Paulina Mkama, amesema tuzo hizo zinahusisha jumla ya washindani 85 kutoka sekta za umma na binafsi, zikilenga kutambua na kusherehekea ubora wa huduma, kuhamasisha ushindani na kutoa fursa kwa wadau na watalii kupigia kura vivutio bora duniani.

Paulina ameeleza kuwa ushiriki wa Tanzania katika tuzo hizo ni fursa adhimu ya kuitangaza nchi kimataifa na kuiweka katika ramani ya dunia kama kitovu cha utalii.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here