TUMIENI BANDARI YA MTWARA KUSAFIRISHA MIZIGO-NAIBU WAZIRI KASEKENYA

Na Siti Said, WUU

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhandisi Godfrey Kasekenya, amewataka wasafisrishaji kutumia Bandari ya Mtwara kwa ajili ya kusafirisha mizigo yao ndani na nje ya nchi ili kunusuru barabara barabara ya Lindi – Kibiti kuharibika mara kwa mara.
Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya, akisisitiza jambo wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum Anastazia James Wambura, jijini Dodoma, kuhusu ubovu wa barabara ya Kibiti – Lindi na mpango wa Serikali unaochukuliwa kutatua tatizo hilo.

Ameyasema hayo Bungeni jijini Dodoma, alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum Anastazia James Wambura, lililouliza ni nini sababu ya barabara ya Kibiti hadi Lindi kuharibika mara kwa mara licha ya kufanyiwa ukarabati, Je, Serikali ina mpango gani wa kutatua tatiza hilo ili kuzuia ajali za mara kwa mara katika barabara hiyo?.

Kasekenya amefafanua kuwa kwa sasa Barabara ya Lindi hadi Kibiti inapitisha magari mengi na yenye uzito mkubwa zaidi ya ilivyokusudiwa wakati wa usanifu uliotumika kujenga barabara hiyo na kwamba hali hiyo inatokana na uwekezaji mkubwa wa viwanda na migodi katika mikoa ya Kusini na nyanda za juu Kusini uliojitokeza miaka ya hivi karibuni baada ya ujenzi wa barabara hii kukamilika.

“Ujenzi wa viwanda vikubwa kama cha Dangote mkoani Mtwara na uwepo wa migodi mikubwa ya Makaa ya Mawe mkoani Ruvuma kumechangia ongezeko la magari yanayobeba uzito mkubwa kuliko ilivyotarajiwa wakati barabara hii inafanyiwa usanifu,"amesema Kasekenya.

Naibu Waziri huyo ameliambia Bunge kuwa ili kukabiliana na changamoto ya uharibifu wa barabara hiyo kwa sasa, Serikali inaendelea na mpango wa ukarabati mkubwa utakaowezesha barabara hiyo kustahimili wingi na uzito wa magari.

Katika mwaka wa fedha 2021/22 zaidi ya shilingi Bilioni Saba zimetengwa kwa ajili ya ukarabati wa barabara ya Lindi hadi Kibiti.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news