Huu ndiyo ujumbe aliouacha marehemu Dkt.Anna Elisha Mghwira

Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira amefariki dunia leo Alhamisi Julai 22, 2021 katika Hospitali ya Mount Meru mkoani Arusha alipokuwa akipatiwa matibabu. 
 
Wiki moja iliyopita alikuwa amelazwa katika Hospitali ya Nkoaranga kwa tatizo la kupumua ambapo baadaye hali yake ilizidi kuwa mbaya na alihamishiwa Hospitali ya Mount Meru.Mwaka mmoja uliopita, akiwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Dkt. Anna Mghwira alitangaza kukutwa na maambukizi ya virusi vya Corona baada ya kufanyiwa vipimo.Unaweza kusoma;BREAKING NEWS:Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Dkt. Anna Elisha Mghwira afariki

Mghwira wakati huo alisema kuwa, hakufahamu amepata wapi na lini maambukizi hayo. Lakini alisema kuwa alikuwa hana dalili zozote na aliamua tu kupima kujua afya yake.

Salamu za rambirambi

Wakati huo huo, Rais Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za rambirambi kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki kufuatia kifo cha aliyewahi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira kilichotokea leo katika hospitali ya rufaa ya Mount Meru mkoani Arusha alipokuwa akipatiwa matibabu.

Rais Samia amesema amepokea taarifa za kifo cha Anna Mghwira kwa majonzi na masikitiko makubwa, hasa akikumbuka mchango wake mkubwa alioutoa katika ujenzi wa Taifa.
Amewaomba Wanafamilia wote wawe na moyo wa uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha majonzi na amemuombea marehemu Anna Mghwira apumzike mahali pema peponi, Amina.

Post a Comment

0 Comments