Balozi Buriani atoa wito kwa Wahitimu wa JKT Operesheni Samia Suluhu

NA TIGANYA VINCENT, TABORA

WAHITIMU wa Mafunzo ya Awali ya Kijeshi wa Jeshi la Kujenga Taifa Msange JKT kwa mujibu wa Sheria chini ya operesheni Samia Suluhu wametakiwa kuwa mfano wa uzalendo na kuigwa watakapojiunga na vyuo mbalimbali hapa nchini.

Kauli hiyo imetolewa leo na Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Balozi Dkt. Batilda Buriani wakati akifunga mafunzo ya awali ya Kijeshi ya miezi mitatu kwa vijana wa Jeshi la Kujenga Taifa Msange JKT kwa mujibu wa Sheria chini ya operesheni Samia Suluhu.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Buriani akikagua leo Gwaride la Wahitimu wa mafunzo ya awali ya Kijeshi ya miezi mitatu kwa vijana wa Jeshi la Kujenga Taifa Msange JKT kwa mujibu wa Sheria ambayo yamepewa jina la Oporesheni Samia Suluhu.

Amesema, wawapo vyuoni wanatakiwa kuwa mabalozi kwa kuonyesha na kuendeleza uzalendo waliofundishwa Msange JKT ili wawe tofauti na Vijana ambao hawakubahatika kupata mafunzo.

Mkuu wa Tawi la Mafunzo na Operesheni kutoka Makao Makuu ya Jeshi la Kujenga Taifa Kanali Aisha Matanza alisema wahitimu hao wanatakiwa kuwa macho na masikio ya Watanzania dhidi ya maadui wa ndani na nje wa Tanzania.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Buriani ( wa pili kutoka kushoto) akipokea salamu leo kutoka kwa Maafisa wa Jeshi kwenda kufunga mafunzo ya awali ya Kijeshi ya miezi mitatu kwa vijana wa Jeshi la Kujenga Taifa Msange JKT kwa mujibu wa Sheria yanayojulikana kama operesheni Samia Suluhu.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Buriani ( katikati waliokaa ) akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa wa Jeshi baada ya kufunga leo mafunzo ya awali ya Kijeshi ya miezi mitatu kwa vijana wa Jeshi la Kujenga Taifa Msange JKT kwa mujibu wa Sheria ambayo yaliyopewa jina la Oporesheni Samia Suluhu.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Buriani (aliyesimama ) akizungumza na Maafisa wa Jeshi kabla kufungwa leo kwa mafunzo ya awali ya Kijeshi ya miezi mitatu kwa vijana wa Jeshi la Kujenga Taifa Msange JKT kwa mujibu wa Sheria ambayo yamepewa jina la Oporesheni Samia Suluhu.

Amesema, wantakiwa kutumia mafunzo hayo kwa ajili ya maslahi ya Nchi na Watanzania na kuwa tayari kuitumikia nchi katika maeneo mbalimbali kwa uzalendo.

Kamanda wa Kikosi cha Msange JKT, Kanali Sadick Mihayo amesema wahitimu hao walianza mafunzo Mwezi Juni mwaka huu wakiwa 1,533 lakini walifanikiwa kuhitimu ni 1,503.

Amesema, katika cha mafunzo wahitimu hao wamefundishwa kozi za awali za kijeshi, shughuli za ujenzi , ujasiriamali kama vile utengezaji wa sabuni , ufugaji wa nyuki , michezo , maandalizi ya mashamba na shughuli za utamaduni.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Buriani akipokea salamu kutoka kwa Wahitimu wa mafunzo ya awali ya Kijeshi ya miezi mitatu kwa vijana wa Jeshi la Kujenga Taifa Msange JKT kwa mujibu wa Sheria ambayo yamepewa jina la Oporesheni Samia Suluhu.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Buriani akihutubia leo wakati wa kufunga mafunzo ya awali ya Kijeshi ya miezi mitatu kwa vijana wa Jeshi la Kujenga Taifa Msange JKT kwa mujibu wa Sheria ambayo yamepewa jina la Oporesheni Samia Suluhu.
Kamanda wa Kikosi cha Msange JKT Kanali Sadick Mihayo akitoa taarifa fupi leo wakati wa ufungaji wa mafunzo ya awali ya Kijeshi ya miezi mitatu kwa vijana wa Jeshi la Kujenga Taifa Msange JKT kwa mujibu wa Sheria ambayo yamepewa jina la Oporesheni Samia Suluhu. (Picha na Tiganya Vincent)

Kanali Mihayo amesema, mafunzo hayo yamewajengea uwezo wa kufanya shughuli mbalimbali za kujitegemea.

Akisoma risala kwa niaba ya wenzake Caroline Tibamanya aliiomba Serikali kuongeza muda wa mafunzo kwa Mujibu wa Sheria ili wahitimu wengi waweze kunufaika na elimu inayotolewa na JKT.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news