MZEE NGONYANI KUZIKWA LEO KIJIJINI KWAKE KWAMNDOLWA SAA 10 JIONI

Na Yusuph Mussa, Korogwe

ALIYEKUWA Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Korogwe mkoani Tanga, Hillary Ngonyani (72) anatarajiwa kuzikwa leo Septemba 10, 2021 katika Kijiji cha Kwamndolwa, Kata ya Kwamndolwa katika Halmashauri ya Mji Korogwe.
Kwa mujibu ya mmoja wa watoto wa mzee Ngonyani, Idd Kabwele, ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Magunga, alisema msiba upo nyumbani kwake Mtaa wa Memba, na maziko yatafanyika leo, ambapo baada ya kuswaliwa mara baada ya Swala ya Ijumaa katika Msikiti Mkuu wa Ijumaa mjini Korogwe, msafara utaelekea kwenye Kijiji cha Kwamndolwa, Kata ya Kwamndolwa kwa maziko.Zinazohusiana unaweza kusoma hapa

Ngonyani amefariki dunia Septemba 9, 2021 saa 9.15 alasiri akiwa nyumbani kwake Mtaa wa Memba mjini Korogwe akiwa kwenye hatua za mwisho kabla ya kumpeleka Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Kwa mujibu wa mmoja wa watoto wake, Richard Ngonyani, alisema mzee Ngonyani alikuwa amelazwa Hospitali ya Wilaya ya Korogwe, Magunga hadi asubuhi ya Septemba 9, 2021 akiwa anasumbuliwa na Nirmonia.

Na tayari saa nne asubuhi ya jana walikuwa wamekamilisha rufaa hiyo ikiwa tayari pia wamepata gari la wagonjwa (Ambulance), hivyo wakamtoa Magunga na kumpeleka nyumbani kwake kwa ajili ya maandalizi ya kwenda Muhimbili.

Richard anasema mara ghafla wakaona amezidiwa na kufariki saa 9.15 alasiri.

Mzee Ngonyani amekuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Mdogo wa Korogwe mwaka 2000 hadi 2005 mji huo ulipopandishwa hadhi na kuwa Halmashauri ya Mji Korogwe mwaka 2004.

Ngonyani amekuwa Diwani wa Kata ya Kwamndolwa tangu mwaka 2000 hadi mwaka 2020 baada ya kushindwa na Neema King'oso kwa kura nne kwenye uchaguzi wa kura za maoni za Chama cha Mapinduzi (CCM), ambapo Neema alipata kura 42, huku yeye akipata kura 38.

Ngonyani ambaye ni kaka wa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini marehemu Stephen Ngonyani maarufu kama Majimarefu, alikuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Korogwe kwa miaka 10 tofauti.

Alikuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Korogwe 2005-2010, Kabla ya kuangushwa na Angelo Bendera, aliyekuwa Diwani wa Kilole. Lakini alirudi tena kwenye kiti hicho mwaka 2015 hadi 2020.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news