RC Kunenge apokea muongozo maalum wa mafunzo ya kuzuia na kupambana na rushwa nchini

NA ROTARY HAULE

Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Abubakar Kunenge, amepokea muongozo maalum wa mafunzo ya kuzuia na kupambana na rushwa nchini kupitia vijana wa skauti waliopo Shule za Msingi na Sekondari Tanzania Bara.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Abubakar Kunenge wa pili kutoka kulia akipokea muongozo wa kufundisha masuala ya kuzuia na kupambana na rushwa shuleni, wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Pwani,Suzana Raymond na wa pili kushoto ni Kamishna wa Skauti Mkoa wa Pwani, Safi Shaban na kwanza kulia ni afisa elimu Mkoa wa Pwani, Sara Mlaki hafla hiyo imefanyika leo katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa iliyopo Kibaha Mjini. (NA ROTARY HAULE).

Kunenge amepokea muongozo huo leo ofisini kwake Mjini Kibaha kutoka timu maalum ya viongozi wa kupambana na kuzuia rushwa Mkoa wa Pwani akiwemo afisa elimu mkoa, Sara Mlaki,Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Pwani, Suzana Raymond pamoja na kamishina wa skauti wa Mkoa wa Pwani, Safi Shaban.

Awali akizungumza kabla ya kukabidhi muongozo huo kwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani, afisa elimu wa mkoa huo, Sara Mlaki,amesema kuwa mafunzo hayo yamelenga kukomesha vitendo vya rushwa Tanzania Bara.

Mlaki amesema kuwa, mafunzo hayo yatakuwa endelevu kwani yataendeshwa na Chama cha Skauti kama programu za kila siku shuleni kupitia vipindi vya skauti.

Amesema kuwa,mafunzo hayo yatajikita katika mambo makubwa matatu ikiwemo uzalendo,utii,uaminifu na kwamba wizara mbili ikiwemo ya Tamisemi na Wizara ya Nchi ,Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora zinashiriki kikamilifu kufanikisha mpango huo.

Amesema,uzinduzi wa programu hiyo ulifanyika Septemba 23, 2021 jijini Dodoma kwa kuwashirikisha maafisa elimu mkoa, Wakuu wa Takukuru wa mikoa na makamishna wa skauti.

Akizungumza mara baada ya kupokea muongozo huo Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge,ameshukuru kupewa muongozo huo huku akisema lazima mkoa uanze kujenga misingi imara toka chini hasa katika kupambana na vitendo vya rushwa.

Kunenge amesema kuwa, anaamini kwenye mafunzo yataleta mafanikio hasa katika kuanzisha klabu hizo huku angependa mkoa huo juu kwa kila jambo.

Ametaka kila taasisi inayopata jambo lazima ilibebe na kushirikisha taasisi nyingine ili kusudi mafanikio yapatikane kwa urahisi.

"Nimepokea muongozo huu na hakika nimeupenda, kwa hiyo ni lazima jambo hili tulisimamie kwas sababu ni msingi mzuri na hata baadhi ya watendaji wanakabiliwa na changamoto hii ya kutokana na mambo haya ya rushwa,"amesema Kunenge.

Hata hivyo, Kunenge ameahidi kuupitia muongozo huo na baadae kuweka utaratibu maaalum wa namna ya kukutana na makundi yote yanayohusika katika mpango huo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news