LESCO yaaswa kuzingatia misingi ya majadiliano ya utatu

NA MWANDISHI WETU

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama ameuasa uongozi wa Baraza la Kazi, Uchumi na Jamii (LESCO) kuzingatia mfumo wa majadiliano kwa kuzingatia utatu ili kuendelea kuleta tija kwa jamii inayoihudumia.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akihutubia wakati wa ufunguzi wa kikao cha Kikao cha Baraza la Kazi, Uchumi na Jamii (LESCO) kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Dodoma tarehe 03 Novemba, 2021 Dodoma.

Ameyasema hayo wakati akifungua kikao cha siku mbili cha Baraza hilo kilichohusu uzinduzi rasmi wa baraza jipya na kuwajengea uwezo wajumbe wa Baraza linalotarajiwa kuhudumu kwa kwa miaka mitatu kwa mujibu wa sheria.Kikao kilifanyika mapema hii leo Novemba 3, 2021 Jijini Dodoma.

Waziri Mhagama alieleza ni lazima kuendelea kufanya kazi kwa weledi na ufanisi kwa kuzingatia mchango wa baraza hilo katika masuala ya jamii, uchumi na ajira nchini.

“Muundo wa Baraza unajumuisha wawakilishi wa Utatu na zaidi (Tripartite Plus) ambao ni Wajumbe wanaowakilisha maslahi ya Serikali, Waajiri, Wafanyakazi na Wajumbe wanaoteuliwa kwa kuzingatia utaalam wao,”alisema Waziri Mhagama.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama pamoja na Naibu wake (Kazi, Vijana na Ajira) Mhe. Patrobas Katambi wakiwa katika kikao cha Kikao cha Baraza la Kazi, Uchumi na Jamii (LESCO) kilichofanyika Dodoma hotel.

Aliongezea kuwa, upo umuhimu wa kuzingatia misingi ya majadiliano ya utatu kwa ajili ya kuleta ufanisi na tija katika utekelezaji wa majukumu ya Baraza.

“Kimsingi, Muundo huu unakidhi matakwa ya Mkataba wa Shirika ka Kazi, ILO Na. 144 wa mwaka 1976 kuhusu Mashauriano ya Utatu (The Tripartite Consultation International Labour Standards) Convention No. 144 of 1976 ambao nchi yetu imeuridhia tarehe 30 Mei, 1983,”Alisisitiza Waziri Mhagama.

Waziri alilitaka baraza hilo kuhakikisha linatekeleza majukumu yake kwa ufanisi ikiwemo la kumshauri Waziri mwenye dhamana ya masuala ya kazi na ajira kuhusu masuala ya Sera ya Soko la Ajira nchini, mapendekezo yeyote kutunga sheria kabla hayajawasilishwa kwenye kikao cha Baraza la Mawaziri, hatua za kuchukua kupunguza tatizo la ajira nchini na masuala yote ya ajira katika ngazi ya kikanda na kimataifa.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri (Sera, Bunge, Uratibu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Bw. Tixon Nzunda akitambulisha wajumbe wa Kikao cha Baraza la Kazi, Uchumi na Jamii (LESCO) kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Dodoma.
Mkurugenzi wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) kwa nchi za Afrika Mashariki, Wellington Chibebe akizungumza wakati wa kikao hicho.
Mwenyekiti wa Baraza la Kazi, uchumi na Jamii (LESCO) Dkt. Samuel Nyantahe akitoa salamu wakati wa kikao cha Baraza hilo.
Mjumbe wa kikao cha Kikao cha Baraza la Kazi, Uchumi na Jamii (LESCO) Dkt. Aggrey Mlimuka akichangia jambo wakati wa kikao hicho.

Aidha kuendelea kumshauri waziri kuhusu masuala ya kijamii na kiuchumi, kufuatilia na kushauri katika mabadiliko ya kisera ili kuendana na mabadiliko ya kidunia yanayotokea mara kwa mara.

Akitoa salamu wakati wa kikao hicho Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waajiri Nchini (ATE), Bi.Suzzane Ndomba alisema uwepo wa Baraza hilo utaleta majadiliano ya pamoja kama sheria inavyoeleza ili kukidhi malengo ya kuundwa kwake, na kuendelea kumshauri waziri mwenye dhamana ya masuala ya kazi na ajira, nchini.

“Chama cha Waajiri nchini kitaendelea kutoa ushirikiano katika kutekeleza majukumu ya baraza hili kwa kuzingatia sheria zilizopo kwa maslahi mapana ya nchi,”alisema Suzzane.
Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) Bi.Suzzane Ndomba akitoa salamu wakati wa kikao cha kikao cha Kikao cha Baraza la Kazi, Uchumi na Jamii (LESCO) kilichofanyika Jijini Dodoma.
Baadhi ya wajumbe wa Kikao cha Baraza la Kazi, Uchumi na Jamii (LESCO) wakifuatilia kikao hicho. (PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU).

Akitoa neno la shukrani Mwenyekiti wa Baraza hilo Dkt. Samuel Nyantahe alimpongeza waziri kwa kuunga mkono jitihada za baraza hilo huku akiahidi kuendelea kuongoza baraza kwa ufanisi, weledi na kuzingatia utatu ili kuyafikia malengo ya uwepo wa baraza hilo.

“Tunashukuru kwa kuendelea kutuunga mkono tunaahidi tunayachukua maagizo yako kama yalivyo na tutayatekeleza ipasavyo, asante kutuongezea nguvu na tunaamini baraza litafanya kazi vizuri zaidi, tunaendelea kuahidi tutachapa kazi ambayo itakushangaza,”alisema Dkt. Nyahtahe

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news