Mbunge Kiteto aeleza fedha walizotengewa na Serikali

NA MOHAMED HAMAD

Mbunge wa Jimbo la Kiteto, Wakili Msomi Edward Ole Lekaita amesema, fedha zilizotengwa na Serikali kwa ajili ya miradi ya maendeleo wilayani humo zitasimamiwa kikamilifu ili zilete tija kwa wananchi.
Alisema Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto imetengewa fedha za miradi ya maendeleo kwa ajili ya ukamilishaji madarasa (maboma) ya shule za Msingi.

Akizungumza hayo Ole Lekaita amesema fedha hizo zimefika wakati mwafaka ambao wana Kiteto wanakabiliwa na changamoto nyingi za kimaendeleo na kudai zitachochea maendeleo na upatikanaji wa huduma kwa wananchi

Alisema, fedha hizo ni kwa ajili ujenzi wa Sekondari, Zahanati pamoja na Kituo cha Afya cha Engusero Jengo la Wadi ya Wazazi mil 200,000,000.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Kiteto, Papakinyi Kaai na Afisa Elimu Msingi.

Ujenzi wa vyumba vya madarasa 9 vya thamani ya milioni 112,500,000 kwa ajili ya kutatua kero za upungufu wa vyumba vya madaraka katika shule za Sekondari Njoro, Kijungu, Dongo na Orkine.

Ujenzi wa vyumba vya madarasa vyumba 9 milioni  112,500,000 kwa ajili ya kutatua kero za upungufu wa vyumba vya madaraka katika shule za Msingi za Mdunku, Ndilali, Loltepesi, Logoet, Kiperesa, Mwitikira, Nalangitomon, Ilera na Songambele

Pesa za kumalizia ujenzi wa zahanati 3 Kijiji cha Njia Panda, Ndirigish na Matui mil 150,000,000.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto, Abdalah Bundalah.

Kukamilisha Ujenzi wa vyumba 5 vya Maabara shule za Sekondari za Ndedo, Dongo, Kijungu, Kiperesa na Njoro mil 75,000,000

Mhe Ole Lekaita alisema jumla ya pesa hizo toka Serikali kwaajili ya miradi tajwa ni 650,000,000

Alisema kwa niaba ya wananchi wa Jimbo la Kiteto, anamshukuru Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan na wasaidizi wake kwa kugusa maisha ya wana Kiteto kuboresha Sekta ya Afya, Elimu kwa kiwango cha juu.

Alisema ahadi kwa Mhe. Rais ni kuzisimamia Fedha hizo ili zitoe matokeo makubwa yenye ufanisi na tija.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news