Salamu za pole alizotuma Rais Dkt. Mwinyi kwa Rais mstaafu Dkt. Shein kufuatia kifo cha kaka yake

NA MWANDISHI MAALUM

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi ametoa salamu za pole kwa Rais Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Awamu ya Saba, Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein kufuatia kifo cha Kaka yake Mzee Shein Mohamed Shein kilichotokea jana Novemba 14,2021.
Katika salamu hizo za pole, Rais Dkt. Mwinyi ameeleza kusikitishwa kwake na kifo hicho na kumtakia pole na ustahamilivu Rais Mstaafu Dkt. Shein yeye na familia yake katika kipindi hiki kigumu cha msiba.

Rais Dkt. Mwinyi na familia yake wamemuomba Mwenyezi Mungu amjaalie Marehemu Mzee Shein Mohamed Shein amlaze mahali pema peponi, Amin.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kitengo cha Habari-Ikulu leo Novemba 15,2021, Rais Dkt. Mwinyi ametoa salamu hizo akiwa jijini Durban, nchini Afrika Kusini akisihiri ufunguzi wa Mkutano wa Maonesho ya Kukuza Biashara baina ya nchi za Afrika.

Post a Comment

0 Comments