Mradi wa Bwawa la Kufua Umeme wa Maji la Julius Nyerere (JNHPP-MW2115) wafikia patamu, Waziri Makamba atoa maagizo

NA MWANDISHI MAALUM

MRADI wa Bwawa la Kufua Umeme wa Maji la Julius Nyerere (JNHPP-MW2115) unatarajiwa kukamilika bila ongezeko la gharama za ujenzi.
Hayo yameelezwa na Waziri wa Nishati, Mheshimiwa January Makamba, Desemba 7, 2021 alipotembelea eneo la mradi akiambatana na Waziri wa Nyumba Maendeleo ya Makazi na Huduma wa Jamuhuri ya Kiarabu ya Misri, Mheshimiwa Assem Hafez El azar.

Ziara hiyo ilikuwa ya pamoja kati ya Nchi za Tanzania na Jamhuri ya Kiarabu ya Misri ambayo imepokea taarifa ya utekelezaji wa mradi ya mwezi Novemba 2021, inayoonesha kuwa utekelezaji wa mradi unakwenda vizuri.
‘‘Kwa dhamira na malengo ya mradi, na gharama zilizotumika, Serikali ya Tanzania haiwezi kuruhusu mradi huu kutokukamilika, kwa wenzetu wa Misri pia mradi huu ni chachu ya ushirika wenye manufaa kwao, pia nao wako tayari kuhakikisha mradi huu unakamilika kwa faida ya nchi zote mbili,"amesema Waziri Makamba.

Ameelekeza timu ya wataalam toka Wizara ya Nishati pamoja na TANESCO kuangalia changamoto zilizojitokeza na kuzifanyia kazi ili kuhakikisha mradi unakamilika kama, Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hasan alivyowaahidi watanzania.
Naye Mhandisi Assem Hafez El azar, ambaye ni Waziri wa Nyumba Maendeleo ya Makazi na Huduma wa Misri amesema, Serikali ya Misri inawahakikishia watanzania kuwa mradi wa JNHPP ni muhimu kwa nchi zote mbili ili kujenga uhusiano na imani kwa watanzania kuwa Misri ni nchi yenye uwezo wa kutekeleza miradi mingine mikubwa ambayo Tanzania itatazamia kuijenga.
Katika ziara hiyo, Mheshimiwa Makamba aliongozana na Naibu Waziri wa Nishati, wa Tanzania, Mheshimiwa Stephen Byabato, Mkurugenzi wa TANESCO, Maharage Chande pamoja na wataalam mbalimbali kutoka Wizara ya Nishati.

Aidha,wamekagua pia maeneo muhimu ya mradi yanayoendelea kujengwa ambayo ni nyumba ya mitambo, sehemu ya kupokelea umeme pamoja na eneo linapojengwa daraja.
Kukamilika kwa wakati kwa mradi Julius Nyerere kutasaidia nchi kupata umeme wa uhakika, bora na wa gharama nafuu na hivyo kukuza uchumi sambamba na kuongeza ajira kwa wataalamu mbalimbali.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news