Rais Samia afanya uteuzi leo Desemba 23,2021

NA GODFREY NNKO

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa viongozi watatu katika nafasi ya uwenyekiti katika taasisi tatu za Serikali.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Jaffar Haniu, Rais Samia amefanya uteuzi huo leo Desemba 23, 2021.

Mheshimiwa Rais Samia amemteua Mhadhiri Mstaafu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Profesa Othman Chande kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS).

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Profesa Othman anachukuwa nafasi ya Dk Fenella Ephraim Mukangara ambaye uteuzi wake umetenguliwa.

Pia amemteua Mkurugenzi Mstaafu wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), Dkt.Aggrey Kalimwage Mlimuka kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Ushindani (FCC).

Dkt. Mulimuka anachukuwa nafasi ya Profesa Humphrey Moshi aliyemaliza muda wake.

Aidha,amemteua Dkt. Andrew Kutua kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binaadamu (NIMR) ambaye anachukuwa nafasi ya Dkt.Deodatus Mtasiwa ambaye amemaliza muda wake.

Post a Comment

0 Comments