Captain Hamad ataja faida za Uchumi wa Buluu Zanzibar

NA GODFREY NNKO

MKURUGENZI wa Idara ya Maendeleo na Uratibu wa Uchumi wa Buluu Zanzibar, Captain Hamad B. Hamad amesema kuwa, Serikali ya Awamu ya Nane chini ya Rais Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi imedhamiria kutumia Uchumi wa Buluu kuimarisha uchumi wa nchi na wananchi kwa ujumla.
Ameyasema hayo leo Januari 2022 katika mjadala wa Kitaifa juu ya dhana ya Mapinduzi ya Zanzibar na Falsafa ya Uchumi wa Buluu kupitia Zoom. 

Mjadala huo umeratibiwa na Watch Tanzania kwa udhamini wa Benki ya Kilimo Tanzania (TADB) ambapo umewakutanisha viongozi wakuu wa Kitaifa na wadau mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi. Pia mjadala huo ni sehemu ya maandalizi ya shamrashamra za maadhimisho ya miaka 58 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
"Uchumi wa Buluu maana yake kwa ufupi kabisa ni kwamba ni utumiaji wa rasilimali zinazopatikana baharini na fukwe na miundombinu yake katika njia endelevu kwa kuleta ustawi wa jamii pamoja na maendeleo ya Taifa. Hiyo ikiwa ndiyo dhana kubwa zaidi katika Mapinduzi ya Zanzibar katika kuwaletea wananchi ahueni ya maisha na kupeleka uchumi wa nchi mbele,"amesema Captain Hamad. 

"Lakini kwa Afrika utaona kuwa, maana ya Uchumi wa Buluu imeenda mbali zaidi,ni kwamba Uchumi wa Bluu mbali ya rasilimali za bahari, unakuta umechukua pia rasilimali zilizopo katika maji ya ndani ikiwemo mito, maziwa lakini hata maji yaliyopo chini.

"Kwa hiyo, Uchumi wa Buluu Afrika unamaana pana zaidi,kuliko ule wa nchi nyingine na hii ni kwa sababu rasilimali za bahari na maji yaliyopo katika ardhi hatujayatumia vizuri,"amesema.

Pia amebainisha kuwa, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imekuja na hii Sera ya Uchumi wa Buluu ambayo tayari imeonyesha mwelekeo mzuri na mwaka 2021 wametoa nafasi ya watu kuweza kukodi visiwa vidogo vidogo kwa ajili ya kutumia kimaendeleo na nchi kufaidika kupitia visiwa hivyo. 

"Zanzibar shughuli zake ni utalii, uvuvi, bandari na kilimo hivyo mnyororo wa thamani wa uvuvi una ajiliri wanawake wengi,"amesema. 

Mkurugenzi huyo amesema kuwa, Wizara ya Uchumi wa Bluu ina kazi kuu tatu ikiwemo kuhakikisha inaendeleza uvuvi na ufugaji wa baharini.

Pili upatikanaji wa mafuta na gesi kwa ajili ya kuendeleza uchumi na tatu kuratibu ya shughuli zingine sambamba na shughuli za uchumi wa bluu kwa maslahi mapana ya nchi na wananchi wake.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news