Haya ni maono ya WaziriJenista Mhagama kuhusu Utumishi wa Umma na Utawala Bora anaotaka kuujenga

 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama amesema amedhamiria kuimarisha misingi ya utendaji kazi kwenye Utumishi wa Umma ili wananchi wanufaike na huduma zitolewazo na taasisi za umma nchini.

“Tunaona imani kubwa aliyo nayo Mhe. Rais kwa Watumishi wa Umma, hivyo nikiwa ndiye Waziri mwenye dhamana ya kumsadia kusimamia Utumishi wa Umma na Utawala Bora, nitahakikisha Watumishi wa Umma wanafanya kazi kwa bidii na uadilifu ili kuendana na kauli mbiu yake ya KAZI IENDELEE,” Mhe. Jenista amefafanua.

Post a Comment

0 Comments