🔴 LIVE:Simba SC vs Namungo FC nusu fainali Kombe la Mapinduzi

MTANANGE huu unapigwa baada ya mabingwa watetezi wa Kombe la Mapinduzi wenyeji wa Jiji la Dar es Salaam, Yanga SC kuondolewa katika nusu fainali kwa penalti 9-8 na Azam FC.
Azam FC ambao ni mabingwa wa kihistoria wa kombe hilo wameiondoa klabu hiyo kupitia mtanange uliopigwa leo Januari 10, 2022 katika dimba la Amaan jijini Zanzibar.

Mshindi kati ya Simba SC wenyeji wa Jiji la Dar es Salaam dhidi ya Namungo FC ambao ni wenyeji wa Mkoa wa Lindi atajumuika na Azam FC katika fainali hapo Januari 13, 2022.

Post a Comment

0 Comments