Rais Dkt.Mwinyi ashiriki maziko ya mama mzazi wa Makamu wa Rais mstaafu wa Tanzania,Dkt.Mohammed Gharib Bilal

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Alhaj Dkt. Hussein Ali Mwinyi leo ameshiriki maziko ya marehemu Bi Safia Abeid,mama mzazi wa Makamu wa Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Mohammed Gharib Bilal yaliyofanyika huko kijijini kwao Kiboje Mwembeshauri, Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dkt.Hussein Ali Mwinyi akiweka mchanga katika kaburi la marehemu Bi.Safia Abeid, Mama mzazi wa Makamu wa Rais mstaafu wa Tanzania Alhaj Dkt.Mohammed Gharib Bilal, maziko yaliofanyika Kijiji kwao Kiboje Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.(Picha na Ikulu).Makamu wa Rais mstaafu wa Tanzania Alhaj Dkt.Mohammed Gharib Bilal akiweka mchanga katika kaburi la Mama yake Mzazi Marehemu Bi.Safia Abeid,baada ya kuweka mwili wa marehemu maziko yaliyofanyika Kijiji kwao Kiboje Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja leo Januari 4,2022.(Picha na Ikulu).

Viongozi mbalimbali wa vyama vya siasa, dini na Serikali, wananchi pamoja na wanafamilia walihudhuria katika maziko hayo ambapo mapema Alhaj Dkt. Mwinyi aliungana nao katika sala ya kumuombea marehemu iliyosaliwa huko Masjid Jaameh Zinjbaar, Mazizini jijini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dkt.Hussein Ali Mwinyi akiitikia dua ikisomwa na Mufti Mkuu wa Zanzibar,Sheikh Saleh Omar Kabi, baada ya kumalizika kwa Sala ya kuusalia mwili wa Marehemu Safia Abeid Mama Mzazi wa Makamu wa Rais Mstaafu wa Tanzania Alhaj.Dkt. Mohammed Gharib Bilal (kushoto kwa Rais) iliofanyika katika Masjid Jamiu Zinjibar Mazizini Wilaya ya Mjini Unguja, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla na Rais Mstaafu wa Zanzibar Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein ( kulia kwa Rais) Naibu Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Hassan Othman Ngwali, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Alhaj Othman Masoud Othman, Rais Mstaafu wa Zanzibar Alhaj Dkt.Amani Karume na Makamu wa Pili mstaafu Alhaj Balozi Seif Ali Iddi.(Picha na Ikulu).
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dkt. Hussein Ali Mwinyi akijumuika na Wananchi katika maziko ya Marehemu Safia Abeid Mama Mzazi wa Makamu wa Rais Mstaaf wa Tanzania Alhaj Dkt. Mohammed Bilal,Mtoto wa Marehemu Bw. Abeid, Makamu wa Pili wa Rais Mstaafu Alhaj Balozi Seif Ali Iddi,yaliyofanyika katika Kijiji cha Kiboje Wilaya ya Kati Unguja na (kulia kwa Rais) Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Hemed Suleiman Abdulla na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Mhe. Rashid Hadidi Rashid.(Picha na Ikulu).
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dkt.Hussein Ali Mwinyi akitowa mkono wa pole kwa Makamu wa Rais Mstaafu wa Tanzania, Alhaj Dkt.Mohammed Gharib Bilal, kwa kufiwa na Mama yake mzazi marehemu Safia Abeid, baada ya kumalizika kwa maziko hayo yaliyofanyika katika kijiji cha Kiboje Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.(Picha na Ikulu).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news