Ametoa kauli hiyo leo wakati mara baada ya kufanya ziara ya kutembelea ofisi ya Ubalozi huo ikiwa ni muendelezo wa kuzungumza na watumishi na wawekezaji mara baada ya kumalizika kufanyika kwa mkutano wa 50 wa mwaka wa uwindaji wa kitalii uliofanyika katika Jiji la Las Vegas nchini Marekani.
Akizungumza na timu ya Watumishi hao, Dkt. Ndumbaro amempongeza Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Dkt. Elsie Kanza kwa kazi kubwa anayoifanya ya Diplomasia katika tasnia ya biashara na utalii.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro akiwa na ujumbe alioambatana nao kutoka Tanzania akimsikiliza Kiongozi wa Vyama vya Wasafirishaji Watalii wa nchini Marekani, Rumit Mehta katika ofisi za Ubalozi za Tanzania katika ofisi za New York za nchini Marekani ambapo Waziri Ndumbaro pamoja na mengine ameamulika Kiongozi huyo kuja Tanzania kutembelea vivutio vya utalii vilivyoko ukanda wa Kusini.Wengine ni watumishi wa Ubalozi Tanzania nchini Marekani katika ofisi za New York.Ambapo amewataka Wanadiplomasia hao kuwa daraja katika kuwawezesha watalii kuja nchini Tanzania.
Dkt.Ndumbaro amesema, Diplomasia ya Uchumi katika tasnia ya utalii inapaswa kutangaza na kujibu maswali ya watu mbalimbali wanaotaka kutalii Tanzania kuhusu namna ya kufika nchini kiujumla na katika kila kivutio cha utalii kimahususi.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro akiwa na ujumbe alioambatana nao kutoka Tanzania akiwa kwenye picha ya pamoja na Watumishi wa Ubalozi wa Tanzania katika ofisi za New York za nchini Marekani mara baada ya kikao kilichofanyika baina yao ambapo ametoa wito kwa watumishi hao kutekeleza Diplomasia ya Uchumi ipasavyo, Wa nne kulia ni kiongozi Vyama vya wa Wasafirishaji Watalii wa nchini Marekani, Rumit Mehta.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro akiwa kwenye picha pamoja na Kiongozi wa Vyama vya Wasafirishaji Watalii wa nchini Marekani, Rumit Mehta wakiwa wameshika picha ya twiga katika ofisi za Ubalozi za Tanzania nchini Marekani katika ofis za New York mara baada ya kumaliza kikao kilicholenga kuimarisha ushirikiano kwenye sekta ya utalii.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro akiwa katika picha ya pamoja na Watumishi wa Ubalozi wa Tanzania katika ofisi za New York za nchini Marekani mara baada ya kikao kilichofanyika baina yao ambapo ametoa wito kwa Watumishi hao kutekeleza Diplomasia ya Uchumi ipasavyo, Wa nne kulia ni kiongozi Vyama vya wa Wasafirishaji Watalii w nchini Marekani, Rumit Mehta.Katika hatua nyingine, Dkt. Ndumbaro amemwalika nchini Tanzania, Kiongozi wa Vyama vya Waongoza Watalii nchini Marekani, Rumit Mehta kuja kutembelea vivutio vya utalii vilivyoko Ukanda wa Kusini.
