Waziri Balozi Mulamula ateua wajumbe Baraza la Uongozi wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC)

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb) kwa mamlaka aliyonayo amefanya uteuzi wa Wajumbe wa Baraza la Uongozi wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC).
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula. (Picha na Maktaba). 

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ambapo uteuzi huo ni kama ifuatavyo:Sethi Mburawabo Kamuhanda, Balozi Mstaafu Daniel Ole Njoolay., Bw. Faustine Ilobi Masalu, Bi. Beatrice Modest Kessy,Bw Patrick Magologonzi Mongella na Bi. Elimbora Abia Muro. 

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na wizara, uteuzi wa wajumbe hawa ni kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia tarehe 28 Desemba, 2021.

Post a Comment

0 Comments